Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia,mti wa ajabu

Hikaya za Anatolia

Leo katika hikaya za Anatolia tunakuleteeni historia ya mti wenye asilia mbili za Linden na mkuyu.Mti huo unapatikana Ege katika mji wa Bergama.Mti huo ni wa miaka mingi na kumekuwa na hikaya tofauti kufuatia kuwepo kwa mti huo.

Hapo zamani za kale sehemu za Ugiriki mungu Zeus alikuwa katika mlima mmoja na kujisikia kuwa hana kitu cha kufanya na ni mpweke.Basi alimuita mungu wa wajumbe Hermes na kumwambia kuwa anaonaje iwapo watafanya jambo ambalo halitawafanya wajisikie wapweke.Basi miungu hao wawili waliamua kutafuta nguo za kibinadamu na kuvaa ili waweze kujificha asili yao.Miungu hao wawili walivaa nguo hizo na kuelekea katika kijiji kimoja cha Anatolia.Kijiji hicho kilikua kinajulikana kwa jina la Frugia na kulikuwa kuna binadamu wakiishi kawaida.Walipofika katika kijiji hicho walianza kugonga kila mlango wakitegemea kukaribishwa kama ilivyokuwa mil ana desturi za watu wa Anatolia.Wageni walikuwa wakithaminiwa sana enzi hizo na ilikuwa ni jambo jema sana kumkaribisha mgeni na kumpa zawadi au takadum.

Basi mungu hao wawili walipokuwa wakigonga nyumba tofauti walishangazwa kuona hamna nyumba hata moja iliyowafungulia mlango wala kuwakaribisha ndani.Waligonga nyumba karibu zote lakini wenyeji waliwatazama na hakuna aliyewaambia hata karibuni.Hilo lilikuwa ni jambo la ajabu kwani katika zama hizo mgeni alichukuliwa kama mfalme.Basi miungu hao wawili walizidi kutembea mpaka mwisho wa kijiji na kuona nyumba moja mbaya na imechoka sana.Walipogonga cha kushangaza walifunguliwa mlango na bibi mmoja na babu na kukaribishwa ndani.Wazee hao wawili waliwakaribisha na kuwapa chakula na vinywaji kama ilivyokuwa utamaduni wa Anatolia.

Miungu hao wawili walishangazwa na harakati hizo na kukaa wamekitizama chakula.Wazee hao walipoona wageni hao hawakigusi chakula wakaanza kûhisi kabisa kame huenda wakawa sio binadamu kama wao.Wazee hao walipatwa na hofu kubwa.Miungu hao walipoona hivyo wakaamua kujitambulisha.Wazee hao walipigwa butwaa kusikia kuwa wamekaribisha miungu nyumbani kwao.Waliwaomba msamaha kama itakuwa kuna kosa lolote watakalokuwa wamefanya.Basi Zeus aliwaita nje na kuwaambia kuwa ameshangazwa na kufurahishwa na adabu waliyokuwa nayo kwa wageni kwani ametembea kijiji kizima na hakuna aliyemkaribisha.Aliwaita wazee hao wawili na kutembea nao hadi kilimani kisha akawaambia wageuke nyuma na kutizama nyumba yao.

Walipogeuka walikuta nyumba yao imegeuka kuwa hekalu kubwa na nzuri.Hawakuamini macho yao.Zeus akawaambia waseme wanachotaka atawafanyia kwani wamemfurahisha sana.Basi wazee wale wawili walimtizama mungu Zeus na kusema kuwa wao wamekuwa pamoja kama mke na mume kwa miaka mingi sana na hivyo hawataweza kukaa bila mmoja wao.Walimuomba Zeus kuwa wangependa wafe kwa pamoja.Namna hiyo hakuna atakaemuona mwenzake anakufa.Basi mungu Zeus aliwakubalia ombi lao na siku ya kufa walikufa kwa wakati mmoja.Walizikwa sehemu moja na juu yao mti huo ulipandwa.Mti huo nusu nim kuyu na nusu ni wa linden.Mpaka leo katika mji wa Bergama hadithi hio inahadithiwa kama ishara ya kuonyesha kuwa mapenzi ya kweli yalikuwepo enzi hizo.

Tukutane tena wiki lijalo kwa hikaya motomoto za Anatolia.


Tagi: mti , hikaya , Anatolia

Habari Zinazohusiana