Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia

Leo katika hikaya za Anatolia tunawaleteeni hadthi ya aliyekua wa kwanza kuvumbua pesa katika eneo la Izmir wakati wa zama za Lidya.Wakati huo kulikuwa na msichana buibui.

Hapo awali kabla ya kuwepo kwa ukristo kulikuwa na mji uliojulikana kwa jina la Colophon kusini mwa Izmir.Mji huo ulikuwa unajulikana kwa kuwa na ubunifu wa kila namna na mara nyingi watu wa pale walikuwa wakitumia ujuzi wao na sanaa waliokuwa nayo kujikimu kimaisha.Ndani ya mji huo kulikuwa na binnti mbunifu kupita kiasi.

Alikuwa ni mshonaji mahiri kabisa.Alikuwa akizungusha mikono yake huku ameshika sindano yake kwa ubunifu kabisa.Msichana huyo alikuwa amebarikiwa sanaa kiasi kwamba watu wengi walikuwa wakinunua bidhaa zake na si hivyo tu watu kutoka miji mngine walikuwa wakikusanyika mbele yake kumtizama jinsi anavyoizungusha mikono yake katika ufumaji huo.

Binti huyo pamoja na kuwa alikuwa amebarikiwa na kipaji hicho hakupenda kuongea na watu hata kidogo.Watu walikuwa wakijikusanya kumuuliza ni ipi siri ya kuwa na kipaji hicho lakini kame alikuwa akiwatizama tu bila ya kuwapa jibu lolote.Watu wote katika sehemu hiyo alikuwa wameshamjua binti huyo na jinsi asiyopenda kuongea.

Siku moja kundi la watu lilikuja na kumuuliza yule binti kuwa je kipaji hicho cha ushonaji mahiri amepewa na mungu Athena?.Binti yule kusikia hivyo kwa mata ya kwanza aliwatizama na kuwaambia kuwa,"Mimi sijapewa kipaji hiki na mungu yoyote.Sio Athena sio nani.Nimekipata kipaji hiki kwa nguvu zangu na jitihada zangu mwenyewe".Basi mungu athens kusikia hivyo alikasirika sana na kisha kumfuata na kumwambia binti huyo kuwa anapashwa athibitishe kile alichokisema kwa watu

.Basi mashindano ya nguvu yaliandaliwa mahali hapo ambapo bini huyo alishindana katika ushonaji na mungu Athena.Kila mmoja wao aliruhusiwa kuchagua kile akitakacho kufuma na atumie rangi aitakayo.Wote wawili walianza kuonyesha vipaji vyao na Athena alichagua kufuma mugu wa bahari huku binti yule akachagua kumfuma mungu Zeus.Wakati wakiendelea kufuma baba yake na Athena alikasirishwa na kitendo cha binti huyo kumfanyia mzaha mungu Zeus kwa kumfuma na kish akashuka na kumnyakua mkasi aliokuwa akiutumia na kisha kuanza kumpiga nao mpaka binti yule akaanguka chini na kuchomwa chomwa na sindano mwili mzima.

Mwili wote ulianza kuvuja damu na mungu Athena kuona hivyo alisikitika sana na kuamua kumbadilisha binti huyo kuwa buibui kwa jina la Arakhne.Wakati wa zama za Antik buibui huyo alikuwa akitumiwa juu ya pesa za wakati huo hasa katika mji wa Ege.Mpaka sasa hikaya hio inajulikana kama hikaya ya binti buibui.

Tukutane tena wiki lijalo kwa hikaya nyingine moto moto za Anatolia.Habari Zinazohusiana