Uturuki yatarajia kupata watalii milioni 40 mwaka huu

Uturuki imejiwekea malengo ya kupata watalii milioni 40 mwaka huu.

Uturuki yatarajia kupata watalii milioni 40 mwaka huu

Uturuki imejiwekea malengo ya kupata watalii milioni 40 mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa AK mjini Antalya,rais Erdoğan amesema kuwa Uturuki inatarajia kupata watalii milioni 40 mwaka 2018.

"Tunatarajia kupata mapato ya utalii $32 billioni,na tutayafikia malengo hayo",alisema rais Erdoğan.

Ripoti zimeonyesha kuwa idadi ya watalii mjini Antalya imeongezeka kwa asilimia 57 na kufikia milioni 10.5 mwaka 2017.

Antalya inatarajia idadi hiyo kuongezeka mpaka milioni 14 mwaka huu.

Uturuki ilikaribisha takriban watalii milioni 3 katika kipindi cha baridi mwaka huu.


Tagi: Uturuki , Utalii

Habari Zinazohusiana