Uturuki kutoa mafunzo kwa polisi nchini Kenya

Uturuki inatarajia kutoa mafunzo ya kupambana na ugaidi kwa mapolisi nchini Kenya.

Uturuki kutoa mafunzo kwa polisi nchini Kenya

Uturuki inatarajia kutoa mafunzo ya kupambana na ugaidi kwa mapolisi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa habari,Uturuki itashirikiana na Kenya katika kuhakikisha kuwa jeshi la Polisi linapewa mafunzo muhimu.

Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na shirika la TİKA.

Kiongozi wa shirika la TİKA amesema kuwa shirika hilo limekuwa likitoa mafunzo kwa polisi katika mataifa tofauti  ulimwenguni na sasa ni zamu ya Kenya.

Pamoja na ubalozi wa Kenya Uturuki , pande zote mbili zilikubaliana kufanya kazi pamoja, hasa katika mafunzo maalum juu ya uchunguzi wa makosa ya jinai, usimamizi katika mgogoro, kupambana na ugaidi, uhalifu uliopangwa, wizi wa magari, na mambo mengine mengi.Habari Zinazohusiana