"Ushindi wa Çanakkale ndio msukumo wa ushindi wa Uturuki katika mapambano"

Rais Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa ushindi katika vita vya Çamakkale ndio msukumu wa Uturuki katika mapambano

"Ushindi wa Çanakkale ndio msukumo wa ushindi wa Uturuki katika mapambano"

Rais wa Uturuki Recep Tayııp Erdoğana asema kuwa ushindi katika vita vya Çanakkale ndio msukumo wa ushindi katika mapamnao ya Uturuki. Rais Erdoğan mapaema  majira ya asubuhi amefahamisha kuwa jeshi la Uturuki katika operesheni yake dhidi ya ugaidi nchini Syria  limeingia mjina kati Afrin na kupandisha bendera ya Uturuki.

Jeshi la Uturuki kwa ushirikian na jeshi huru la Syria limeingia mjini kati Afrin baada ya kuwafukuza magaidi.

Akiwa katika hafla ya maadhimisho ya mashujaa wa vita vya Çanakkale miaka 103, rais Erdoğan  amewaambia raia kuwa jeshi la Uturuk limeingia mjini  kati Afrin katika operesheni yake iliokuwa na lengo la kuwaondoa magaidi mipakani mwa Uturuki na Syria.

Rais Erdoğan amesema kuwa jeshi la Uturuki limefaanikiwa kuingia mjini kati Afrin kufautia operesheni ilionzishwa Januari 20 mwaka 2018.

Rais Erdoğan ametoa pongezi kwa wanajeshi wa jeshi huru la Syria na jeshi la Uturuki kwa kuingia Afrin na kuwaondoa magaidi.

Magaidi wameondolewa Afrin katika siku ya 56 ya operesheni ya Tawi la Mzaituni tangu kuanza kwake.

Bendera ya Uturuki na ile ya jeshi huru la Syria ndizo zinazopepea Afrin nchini Syria.

 

 

 Habari Zinazohusiana