Raia wa kigeni wasiokuwa na vitambulisho waendelea kukamatwa Uturuki

Wahamiaji haramu 21 wakamatwa wakijaribu kusafiri kinyume na sheria kuelekea nchini Ugairiki

Raia wa kigeni wasiokuwa na vitambulisho waendelea kukamatwa Uturuki


Wahamşai haramu 21 wamekamatwa na kikosi cha Polisi katika operesheni zake za kila siku kukabiliana na wahamaiji haramu wanaotumia fukwe za Uturuki kusafiri kinyume na sheria kuelekea  nchini Ugiriki.
Jeshi la Polisi Muğla limefahamisha kuwakamata wahamiaji haramu 21 wengi wao wakiwa ni raia kutoka Syria.
Watu  hao walikuwa wakisafiri katika lori dogo ambapo dereva wa gari hilo alikamatwa  akishutumiwa kuhusina na maandalizi ya safari hiyo.
Upelelezi unaendelea ili kubainisha kuwa dereva huyo ndie anahusika na uandaaji wa safari hizo kuelekea nchini Ugiriki.
Whamiaji haramu waliokamatwa walipelekwa katika kituo cha uhamiaji kwa lengo la kusajiliwa.Habari Zinazohusiana