Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Haber Türk: « Uturuki  na Marekani kuafikiana kuhusu Manbich»

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu  akiwa mjini Moscow nchini Urusi  ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo kuhusu ushirikiano bain aya Uturuki na Urusi,  amefahamisha kuwa hali kuhus Manbichi  itawekwa wazi  katika mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika ifikapo Machi 19 kwa ushirikiano na viongozi wa  Marekani. Mevlüt Çavuşoğlu amesema kuwa  wanamgambo wa kundi la kigaidi la PKK/YPG  watakapoondolewa  Manbich, usalama utakuwa ukilindwa na na jeshi la Uturuki kwa ushirikiano na jeshi la Marekani.

Sabah: « Uturuki yakemea shambulizi dhidi ya waziri mkuu wa Palestina»

Uturuki imekemea vikali  shambulizi la silaha lililomlenga waziri mkuu wa Mamlaka ya wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Msafara wa  waziri mkuu wa Palestina Rami al Hamdallah ulishambuliwa  na mtu aliekuwa na sialaha Ukanda wa Gaza.  Uturuki inawatakia shifaa majeruhi wa shambulizi hilo na kulaani vikali waliohusika na tukio hilo la uharibifu

Hürriyet: « Ujumbe wa kuridhisha  kwa Uturuki»

Shirika la ushirikiano na maendeleo ya kiuchumi limetoa ripotia yake  kuhusu uchumi  na kufahamisha kuwa linataraji kuongeza  kiwango chake  nchini Uturuki.  Shirika hilo linataraji kuongeza kiwango chake kwa asilimia 6,9  ambapo hapo awali ilikuwa ni asilimia 6,1 mwaka 2017. Mwaka 2018  asilimia 5,1 na mwaka 2019 asilimia 4,7.

Vatan: « Watalii kutoka Uholanzi kutembelea Uturuki»

Aslimia 90  ya watalii kutoka nchini Uholanzi inataraji kutembelea Uturuki katika msimu wa kiangazi ambao huwa ni msimu wa likizo barani Ulaya. Kiwango cha watalii kutoka Uholanzi kinachataka kutalii Uturuki kimeongezeka na kufikia aslimia 90.  Vyombo vya habari nchini Uholanzi vimefahamisha kuwa  mashirika ya kundaa safari  ANVR yanashuhudia ungezeko la wasafiri katika kipindi cha likizo.Habari Zinazohusiana