Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo
Ulimwengu wa michezo 

Rafael Nadal amekuwa mchezaji mzuri wa tenisi kwa miaka mingi.Amekuwa na uwezo wa kuwafunga wacheza tenisi bora wengi uwanjani,katika michezo na mashindano tofauti.Tukitizama msimu huu Nadal ameshindwa na Federer mara nne,hali hio inaweza kutufanya tubadilishe mawazo na kudhani kuwa Federer ndie mchezaji mashuhuri wa tenisi.

Federer amekuwa bingwa wa mashindano ya Grand Slam mara kumi na tisa,akifuatiwa na Nadal aliyeshinda mashindano hayo mara kumi na sita.Nadal hakushiriki michezo mingi msimu huu kutokana na majeraha.Kwasababu ya hali hii ya Nadal,Djokovic amekuwa akishinda katika michezo mingi.
Nadal alipoulizwa ni nani amekuwa mpinzani wake bora,alishindwa kutoa jibu kamili na kusema kuwa akimtaja Federer nayo pia itakuwa sio haki.Mwanamichezo ni mwanamichezo tu....

Tukitizama upande wa soka.Mchezaji maarufu Christiano Ronaldo ameweza kujishindia mpira wa dhahabu mara ya tano na kuchaguliwa kama mchezaji bora.Katika jarida la soka la Ufaransa imeınyeshwa jinsi Ronaldo alivyopata tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka 2008,2013,2014,2016.Baada ya kupata mpira wa dhahabu mwaka huu,Ronaldo sasa yuko sambamba kabisa na Lionel Messi.

Tumtizame mwanariadha Usain Bolt.Mzaliwa huyu wa Jamaica mwenye umri wa miaka 31 ameshinda medali za dhahabu nane katika olimpiki,medali za dhahabu kumi na moja katika mashindano ya ubingwa wa dunia.Baada ya kujinyakulia ubingwa 2017,Usain Bolt ameachia ngazi.

Tutizame mchezo wa miereka kwa wanawake.Katika kitengo cha kilo 75 kuna Yasemin Adar,kilo 85 Metehan Başar,kilo 130 Riza Kayaalp.Yasemin Adar,Metehan Başar na Riza Kayaalp wamejipatia medali za dhahabu katika mashindano yaliyofanyika Paris 21-26 Agosti.Katika mashindano ya Ubingwa Ulaya Talat Akgül amekuwa wa pili huku katika kitengo cha kilo 74 Soner Demirtaş amechukua nafasi ya tatu.

Huku wanamichezo wakiwa wanapewa medali kadha wa kadha kuna baadhi ya wanamichezo wananyakuliwa za kwao kutokana na kukutwa kuwa walishinda baada ya kutumia dawa za kuongeza nguvu.Je tatizo hili,linasababishwa na wachezaji wenyewe au ni makosa ya viongozi wao?.OIC imeitoa Urusi Katika mashindano yajayo katika msimu wa baridi 2018 kutokana na kosa la utumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu.Hata hivyo wale wachezaji watakaokutwa damu zao safi,basi wataruhusiwa kushindana mashindano hayo kivyao.

Mashindano ya Formula 1,ratiba ya mwaka 2018 imetolewa.FIA imetangaza kuwa idadi ya washindani itakuwa ni 21 badala ya 20.Nafasi ya Malaysia itachukuliwa na Ufaransa pamoja na Ujerumani.Mashindano hayo yanatarajia kuanza 25 machi 2018 Grand Prix Australia.Mchezo wa kwanza utafanyika Abu Dhabi.

IAAF nayo imetoa ratiba yake 2018.Mashindano ya bingwa wa Ulaya yataanza kufanyika 4 Februari Ureno.Mashindano ya 17 yatafanyika Uingereza 1-4 Machi.Mashindano ya marathon yatafanyika Uhispania 24 machi.Mashindano ya kutembea yatafanyika China 5-6 May.Mashindano ya kupanda mlima yatafanyika Macedonia 1 Juni.
Mashindano ya 17 ya miaka chini ya 20 yatafanyika 17-30 Juni nchini Finland.Mashindano kabambe ya mwisho wa msimu huo yatafanyika 9 Desemba Holand kati ya nchi 25 za Ulaya za msalaba mwekundu.

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.


Habari Zinazohusiana