Macron ajibu vijembe vya Donald Trump

Macron ajibu vijembe dhidi yake na Ufaransa vilivyotolewa na rais wa Marekani Donald Trump

Macron ajibu vijembe vya Donald Trump

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa mshirika wa Marekani haimaanishi kwamba wanaitegemea nchi hiyo.

Macron aliyasema hayo katika mahojiano ya mojo kwa moja na kituo cha TF1 kama majibu kwa ukosoaji uliofanywa na rais wa Marekani Donald Trump.

Alisema hakutaka kujibu juu ya ukosaji uliofanywa juu ya fikra ya kuanzisha jeshi la Ulaya, akaongeza kwamba rais Trump anafanya siasa ya kimarekani na yeye hawezi kumruhusu aendelee kufanya hivyo.

Rais Macron aliendelea kusema kwamba anaamini katika mamlaka ya Ulaya hivyo hawezi kuweka hatima ya usalama wa wafaransa wote katika mikono ya wamarekani.

Macron alisema wameamua kuandaa bajeti  mpya ya ulinzi na katika hilo watalifanya kwa ngazi ya Ulaya.

"Mara nyingi huwa tunageukia Marekani ambaye ni mshirika wetu wa kihistoria, na itaendelea kuwa hivyo lakini kuwa washirika haimaanishi kutegemeana, inabidi tusiwategemee" alisema Macron.

 

 

 Habari Zinazohusiana