Familia ya mfalme wa Saudia yatoa pole kwa familia ya Khashoggi

Mfalme wa Saudıa Selman bin Abdulaziz na mrithi mstahiki mwana mfalme Muhammed bin Selman watoa pole kwa familia ya mwanahabari aliyeuawa  Jamal Kashoggi

Familia ya mfalme wa Saudia yatoa pole kwa familia ya Khashoggi

Mfalme wa Saudia Salman bin Abdulaziz na mrithi mstahiki mwana mfalme Muhammed bin Salman wametoa pole kwa familia ya mwanahabari msaudia aliyeuawa  Jamal Kashoggi.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na shirika la habari la Saudia (SPA), mfalme na mwanamfalme huyo waliongea kwa njia  ya simu na mtoto wa Khashoggi aitwaye Salah na kumpa pole kwa msiba huo.

Mfalme Salman na mwana mfalme Bin Salman kwa nyakati tofauti wamekutana na familia na watu wa karibu wa Khashoggi na kutoa salamu zao za dhati za rambi rambi kwa msiba huo.

Salah naye alishukuru kwa salamu hizo.

Uongozi wa Saudi ulitangaza kwamba mwanahabari Khashoggi aliuawa Oktoba 2 kutokana na purukushani na vurugu zilizotokea ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul kama inavyofahamishwa rasmi na Suadia. Habari Zinazohusiana