Msikiti mkubwa zaidi Ulaya kuzinduliwa na rais Erdoğan Ujerumani

Rais Erdoğan wa Uturuki anatarajia kuzindua msikiti mkubwa zaidi Ujerumani na Ulaya nzima ifikapo 29 Septemba.

Msikiti mkubwa zaidi Ulaya kuzinduliwa na rais Erdoğan Ujerumani

Rais Erdoğan wa Uturuki anatarajia kuzindua msikiti mkubwa zaidi Ujerumani na Ulaya nzima ifikapo 29 Septemba.

Kiongozi wa Umoja wa Uislamu (DİTİB) Nevzat Yaşar Aşıkoğlu amesema kuwa msikiti huo utakuwa ni ishara ya umoja wa waislamu wanaoishi mahali hapo.

Utakuwa ni msikiti mkubwa zaidi Ujerumani na Ulaya nzima na hivyo kuwapa fursa kubwa waumini wa kiislamu kuitumikia dini yao ipasavyo.

Katika ufunguzi huo,rais Erdoğan atakuwa na viongozi wengine wa Ujerumani.

Msikiti utakuwa na sehemu ya kusalia wanaume na wanawake,Chumba cha mkutano chenye uwezo wa kubeba watu 600,ukumbi wa maonyesho,chumba cha semina,maktaba kubwa kabisa na ofisi za kazi.

Msikiti huo umejengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na utakuwa na sehemu maalumu ya kuegesha magari.Habari Zinazohusiana