Trump aomba kukutana na Rouhani

Rais Donald Trump amesema kuwa angependa sana kukutana na rais wa Iran,Hassan Rouhani

Trump aomba kukutana na Rouhani

Rais Donald Trump amesema kuwa angependa sana kukutana na rais wa Iran,Hassan Rouhani.

Hayo yamezungumzwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo katika kipindi cha televisheni kilichoandaliwa na kituo cha habari cha NBC.

Trump anataka kuonana na Rouhani katika mkutano wa 73 wa Umoja wa Mataifa unaotarajia kufanyika wiki hii.

"Trump siku zote ana hamu ya kukutana na watu",alisema Pompeo.

Kwa upande mwingine,Trump amesema kuwa atahamishia macho yake kwa Iran baada ya kuionya Korea Kaskazini kuachana na silaha za nyuklia.

Kim Jong Un ameamua kuachana na makomboraya nyuklia hasa baada ya kukutana na rais wa Korea Kusini Pyongyang siku chache zilizopita.

 Habari Zinazohusiana