Marekani yaendelea kutoa silaha kwa kundi la kigaidi la YPG/PKK Syria
Marekani yaendelea kutoa silaha kwa kundi la kigaidi la YPG ambalo ni tawi la kigaidi la PKK nchini Syria

Marekani yaendelea kutoa silaha kwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la YPG ambalo ni tawi la kundi la kigaidi la PKK.
Zaidi ya malori 1500 yakiwa na silaha na magari ya kivita yamekabidhiwa wapiganaji ya kundi la YPG katika kipindi cha siku 30.
Marekani inafahamisha kuwa silaha hizo ambazo wanapewa wanamgambo wa kundi hilo la YPG ambalo ni tawi la kundi la PKK ni kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa kundi la Daesh Deir ez-Zor.
Malori yaliokuwa na silaha yameonekana yakivuka mpaka kati ya Irak na Syria yakielekea mjini Deir ez Zor.
Mwanahabari wa shirika la Anadolu amenasa picha za msafara wa malori yaliokuwa yamesheheni silaha.
Marekani imetoa msaada wa kwanza kwa wanamgambo wa YPG tangu Aprili mwaka 2016.