Putin ataka kukutana na Kim Jong Un mapema iwezekanavyo

Rais Vladimir Putin ametangaza kuwa ana nia ya kukutana na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mapema iwezekanavyo

Putin ataka kukutana na Kim Jong Un mapema iwezekanavyo

Rais Vladimir Putin ametangaza kuwa ana nia ya kukutana na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mapema iwezekanavyo.

Kulingana na kituo cha habari cha Korea Kaskazini KCNA,Putin ameonyesha dhamira yake ya kukutana na Kim wakati akiipongeza Korea Kaskazini katika siku ya maadhimisho ya miaka 73 ya uhuru.

"Ninafurahishwa sana na mahusiano mazuri kati ya mataifa haya mawili na nipo tayari kukutana na wewe hivi karibuni ili kujadili masuala muhimu",alisema Putin.

Rais Putin vilevile amesema kuwa na matumaini ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Korea Kaskazini,Korea Kusini na Moscow.

Mnamo mwezi Juni,Putin alimualika Kim katika mkutano wa kimataifa utakaofanyika Vladivostok Urusi mwezi Septemba.

Hata hivyo haijajulikana bado iwapo Kim Jong Un atahudhuria mkutano huo ama la.Habari Zinazohusiana