Erdoğan: "Trump amethibitishi kuwa hakuna tatizo kuhusu kukabidhiwa kwa ndege za F-35 kwa Uturuki"

Rais wa Uturuki asema kuwa rais wa Marekani amemthibitishia kuwa hakuna tatizo lolote kuhudu kukabidhiwa Uturuki ndege aina ya F-35

Erdoğan: "Trump amethibitishi kuwa hakuna tatizo kuhusu kukabidhiwa kwa ndege za F-35 kwa Uturuki"

 

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa rais wa Marekani Donald Trump amemthibitishi kuwa hakuna tatizo lolote lile kuhusu Uturuki kukakbidhiwa ndege za kivita aina ya F-35.

Hayo rais wa Uturukş aliyafahamisha akiwa safarini akijielekeza nchini Uturuki baada ya kushiriki katika mkutano wa jeshi la kujihami la Magharibi NATO uliokuwa ukifanyika mjini Brussels nchini Ubelgiji. Mkutano huo ulichukuwa muda wa siku mbili ambapo masuala tofauti ya ushirikiano baina ya mataifa wanachama  yalijadiliwa.

Rais  Erdoğan amewafahamisha waandishi wa habari katika ndege iliokuwa ikimsafirisha kutoka Ublelgiji kuwa rais Trump amemthibitishia kuwa  hakuna tatizo lolote kwa Uturuki kukabidhiwa ndege zake za kivta iana ya F-35.

Katika mkutano wa NATO kumejadiliwa na kuafikiwa kuwa Uturuki inatakiwa kuongeza uwepo wake nchini Afghanistan.

Uamuzi huo ni kwa ajili yaushirikiano katika kupambana na ugaidi.

 

 


Tagi: F-35 , NATO , Trump , Uturuki

Habari Zinazohusiana