Balozi wa Marekani nchini Canada apata vitisho vya kuuawa

Balozi wa Marekani Canada Kelly Knight Craft  amepokea vitisho vya kuuawa pamoja na barua iliyokuwa na unga mweupe ndani yake iliyotumwa katika nyumba yake Ottawa.

Waziri wa mambo ya nje wa  Canada Chrystia Freeland amemuambia balozi huyo  kuwa jambo hilo halikubaliki hata kidogo.

Katika barua hiyo vilevile,balozi huyo ametakiwa ajiuzulu la sivyo atauawa.

Rais Trump hapo awali alimkashifu waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau kwa kumuita dhaifu na asiyekuwa mwaminifu baada ya kuisha kwa mkutano wa G7 uliofanyika Quebec 7-8 Juni.

Nchi zote mbili zinafanya uchunguzi kufuatia tukio hilo.Habari Zinazohusiana