Shambulizi lililolenga meli ya Uturuki Yemen  halikusababisha maafa

Msemaji wa mambo ya nje wa Uturuki asema kuwa shambulizi la kombora lililolenga meli moja ya Uturuki Yemen halikusababisha maafa yeyote

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Uturuki Hami Aksoy asema kuwa  shambulizi la kombora lililolenga meli ya Uturuki katika bahari ya Yemen halikusababisha maafa.   Hami Aksoy alihojiwa na waandishi wa habari kufuatia shambulizi na kusema kuwa hakana maafa yeyote  yaliosababishwa na shambulizi hilo la kombora.

Meli ya Uturuki ilioshambuliwa inafahamika kwa jina la İnce İnebolu.

Msemaji wa wizra ya mambo ya nje wa Uturuki amesema kuwa  meli hiyo ilikuwa na ngano ikitokea katika  bandari ya  Novorossysk nchini Urusi kuelekea bandari ya Saalef nchini Yemen. Meli hiyo  ilishambuliwa Mei 10  majira ya usiku.

Tagi: ugaidi , Yemen , Uturuki

Habari Zinazohusiana