Trump kufanya ziara Uingereza

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kufanya ziara rasmi nchini Uingereza ifikapo Julai 13.

Trump kufanya ziara Uingereza

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kufanya ziara rasmi nchini Uingereza ifikapo Julai 13.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson ameandika ujumbe huo katika mtandao wake wa kijamii.

Johnson ameonyesha kufurahishwa na ziara ya rais Trump nchini Uingereza.

Trump anatarajia kukutana na waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May.

Wakati wa ziara ya Theresa May nchini Marekani mnamo Januari mwaka jana,Malkia Elizabeth II alimtumia Trump mualiko na ukakubalika.

Hata hivyo baadae wananchi nchini Uingereza waliandamana kupinga kufanyika kwa ziara ya Trump nchini humo na kusema kuwa hawamtaki.

Maandamano hayo yalilazimisha ziara hiyo kuahirishwa.Habari Zinazohusiana