Uturuki yatolea wito Marekani kuacha kuunga mkono makundi ya kigaidi

Uturuki kupitia wizara yake ya shseria imetolea wito seriakli ya Marekani kuacha kuunga mkono makundi ya kigaidi

Uturuki yatolea wito Marekani kuacha kuunga mkono makundi ya kigaidi

Wizara ya sheria ya Uturuki imetoa tamko baada ya kutolewa ripoti kuhusu haki za binadamu iliotolewa na  Marekani. Kwa mara nyingine Uturuki imetolea wito Marekani kuacha  kushirikiana na kutoa usaidizi kwa makundi ya kigaidi. 

Katika taarifa iliotolewa na wizara ya sheria ni kwamba ripoti hiyo imegubikwa na masuala kuhusu taifa moja. Uturuki kwa upande wake imetolea wito Marekani kuacha  kutoa usaidizi kwa  kundi la kigaidi la FETÖ na kundi la kigaidi la PKK na washirika wake PYD/YPG.

Wizara ya sheria ya Uturuki imesema kuwa ripoti hiyo imetumia  matamshi yaliovuka mipaka  na yasiokuwa na nia ya diplomasia. 

 

 


Tagi: YPG , PKK , ugaidi , Uturuki , Marekani

Habari Zinazohusiana