Jens Stoltenberg : Hakuna taifa ambalo limekabiliwa na ugaidi zaidi ya Uturuki

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg asema kuwa hakuna taifa ambalo limekabiliwa na matendo ya kigaidi zaidi ya Uturuki

Jens Stoltenberg : Hakuna taifa ambalo limekabiliwa na ugaidi zaidi ya Uturuki

Katibu  mkuu wa munngano wa mataifa ya Magharibi wa kujihami NATO Jens Stoltenberg amesema kuwa hakuna taifa ambalo limekabiliwa na matendo ya kigaidi zaidi ya Uturuki.

Jens Stoltenberg ametolea wito kuilewa serikali ya Uturuki kwa kuendesha operesheni dhidi ya ugaidi.

Katibu mkuu wa NATO ameyafahamisha hayo  akiwa katika mkutano na tume ya wajumbe wa mambo ya nje wa bunge la Uholanzi. Jens Stoltenberg amesema kuwa Uturuki inawajibika vilivyo katika kupambana na ugaidi na kulinda mipaka ya moja ya taifa mwanachama wa NATO.

Akizungumza kuhusu mgogo na hali ya mvutano iliopo baina ya Uturuki na Ugiriki, Jens Stoltenberg ameseka kuwa mataifa hayo ni  mataifa muhimu katika munngano wa NATO na kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa mataifa hayo ambayo ni majirani kuwa na ushirikiano usikuwa na tofauti za kudumu.

 Habari Zinazohusiana