Rais wa Nigeria kukutana na rais wa Marekani White House

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kukutana na rais wa Marekani Donald Trump katika ziara yake nchini Marekani

Rais wa Nigeria kukutana na rais wa Marekani White House

Rais wa Nigeria Muhammadu Buahari anatarajiwa kufanya zşara yake rasmi nchini Marekani  ifikapo Aprili 30. Katika ziara yake hiyo rasmi rais wa Nigeria atakutana na rais wa Marekani Donald Trump ikulu White House.

Mkutano baina ya rais wa Marekani Donald Trump na rais wa Nigeria umandaliwa baada ya wiki chache  Rex Tillerson kupigwa kalamu.

Rex Tillerson alipigwa kalamu na rais Trump baada ya kufanya ziara katika mataifa kadhaa barani Afrika ikiwemo Nigeria.

Ziara ya Rex ilishuhudiwa baada ya  rais wa Marekani kutoa matamshi makali dhidi ya mataifa ya bara la Afrika kutaja kuwa ni "shimo la choo".

 

 Habari Zinazohusiana