Mtazamo

Kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo  cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL anazungumza kuhusu suala hilo

Mtazamo

Istilahi pia huamua maudhui. Jinsi unavyotizama  suala na msimamo wako juu ya jambo.Ni muhimu jujua unalitizama jambo kama tatizo au suluhisho.

Kupanuka kwa taifa la Israel.

Kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo  cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL anazungumza kuhusu suala hilo ...

Ili tupate uelewa zaidi tuchukue mfano wa  "Uislamu wa wastani" .Hapa tunazungumzia uislamu.Tunazungumzia uislamu usiokuwa na dhana kama jihadi,sheria kali na kadhalika.Lakini bado tunazungumzia Uislamu. Kama vile hapo awali nilipoandika kuhusu Mashariki yenye dhana za wastani zisizozidi na kukithiri.Bado tulikuwa tukizungumzia nchi za mashariki .

Katika uchambuzi kuelekea Mashariki ya Kati, hasa katika mgogoro wa Syria, mambo mawili yenye upungufu huonekana. Kwanza, kuna wakati mwingine uchambuzi katika Mashariki ya Kati unaonyesha hakuna nchi kama Israeli. Kama ilivyo katika mgogoro wa Syria, Israeli inaweza kupuuzwa kama matatizo katika Mashariki ya Kati hayajahusiana na nchi hii. Hata hivyo, baada ya kuanzishwa kwa Israeli, watu wa Mashariki ya Kati labda wamekuwa wakiishi na  wasiwasi zaidi wa historia yao.

Katika mgogoro wa Syria, ushawishi wa Israeli wakati mwingine umesahauliwa.Uendelezi  na malezi ya hali kama hii,umeleta madhara ya ndani katika Mashariki ya kati. Nchi nyingi zinaweza kuhojiwa wakati wa kuzungumza kuhusu Mgogoro wa Syria  tangu mwanzo. Lakini katika mgogoro huo nchi yenye kufaidika ni Israeli. Kwa sababu, pamoja na mgogoro huo, ni kati ya nchi zote ambazo Israeli walihisi kama tishio kwa ardhi iliyopotea. Nchi kama Syria, Iran, Uturuki, nchi za Kiarabu, zinaona uharibifu mkubwa unaoletwa na mgogoro huo. Baadhi ya nchi za Ghuba, ambazo zilikua karibu na Palestina sasa zinaonekana kutengeneza mahusiano na Israel.

 Kwa upande mwingine jamii ya Israeli, haijali mashirika ya haki za binadamu, ukiukwaji wa haki za binadamu, sera kujitanua, wala Syria.

Upungufu wa pili katika uchambuzi, kwa kawaida mbinu hiyo inaeleza kuhusu tatizo la usalama wa Israeli, lakini usisahau Israel inafaidika na mazingira ya mgogoro wa Syria na suala hili linajulikana  maalum Mashariki ya Kati. Wachambuzi wa Magharibi na wakati mwingine wa Mashariki ya Kati hutizama  "usalama Israeli" wakati wa uchambuzi wao. Ukiangalia suala kutoka katika matazamo wa ”Usalama wa Israel”  utaona kwamba mambo yote yaliyofanwa na Israel yanatizamwa kihalali. Kwa sababu kila nchi ni kawaida kuwa na jambo la masuala ya usalama na ni lazima kuchukua hatua muhimu moja kwa moja dhidi ya vitisho kwa nchi yao. Wakati nchi ikichukua tahadhari hizo inaweza kushutumiwa kwa kushindwa kuzingatia sheria na hakii za binadamu.

Hata hivyo shida katika Mashariki ya Kati sio usalama wa Israeli, lakini tatizo la upanuzi wa Israeli. Ramani hii inaonyesha wazi ukweli huu, ambayo mara nyingi huonekana katika vyombo vya habari na inaonyesha jinsi ambavyo Israeli imepanua eneo lake tangu 1947. Mwaka wa 1946, Wayahudi waliishi tu katika baadhi ya makazi katika nchi za Palestina, leo hali hiyo inabadilishwa. Ramani hii ni maelekezo ya wazi na yenye uchungu kwamba kiwango ambacho Wapalestina wamepunguziwa eneo kumewafanya wawe kama gerezani. Mwandishi wa habari Mehmet Akif Ersoy, katika uandishi wake wa "Nini ndoto yako," kijana wa Gaza alijibu na kusema kuwa ndoto yake ni kuendesha gari ndani ya nusu saa kwa kasi ya 180km bila kudhibitiwa na Israel.

Kwa upande mwingine, hakuna ishara kwamba Israeli atabaki kwenye mipaka ambayo inayo leo. Ingawa kulikuwa na Wayahudi fulani dhidi ya vitu vinavyoendelea  kama ubaguzi wa rangi lakini kimsingi ni wazi kuwa Israel ina panua eneo lake na inataka kulifanya taifa lake kuwa lenye nguvu. Utafiti mdogo kwenye mtandao ni wa kutosha kuuona ukweli huu.. Leo mgogoro wa Syria na ubaguzi wa rangi ni mambo yanayoifaidisha Israel. 

Sera ambazo Israel imekuwa ikizitumia toka kuanzishwa kwa taifa hilo kwa sasa zinaonekana kama sera za ukanda.Sera hizo zinaonekana kuficha uovu wa taifa hilo.Kwa kumalizia tu suala sio ”Usalama wa Israel”,suala zima hapa ni ”Kupanuka kwa taifa la Israel”.

Kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit. Dr. Kudret BÜLBÜL alipendekeza tathmini ya suala hilo ..Habari Zinazohusiana