Wanamichezo 13 kutoka barani Afrika watoeka  katika michezo ya Commonwealth Australia

Wanamichezo 13 kutoka  katika mataifa tofauti barani Afrika watoeka na kukwepa kushiriki katika michauano ya Commonwealth yalioandaliwa nchini Australia

Wanamichezo 13 kutoka barani Afrika watoeka  katika michezo ya Commonwealth Australia

Taarifa zinafahamisha kuwa wanamichezo  kutoka nchini Cameroon, Rwanda, Sierra Leone na Uganda  waingia mitini baada ya kuwasili nchini Australia ambapo walijielekeza nchini humo kwa lengo la kushiriki katika michezo ya Commonwealth ya mwaka 2018.

Wanamichezo wengine watano kutoka barani Afrika wameingia mititi nchini Australia Alkhamis baada ya wanamichezo  wanane kutoka Kameruni  kukosekana.

Tume ya wanamichezo kutoka nchini Ghana imethibitisha  kuwa wanamichezo kutoka Rwanda , Uganda na Sierra Leone wametoeka na hawajulikani walipo.
Kiongozi wa michezo wa Commonwealth David Grevemberg amesema kuwa wanamichezo hao wanatafutwa kwa juhudi kubwa kwa ushirikiana na maafisa wa idara ya uhamiaji.

Ruhusa waliopewa wanamichezo kushiriki katika michezo hiyo nchini Australia itamalizika Mei 15 huku waziri wa masuala ya familia Peter Dutton akiwaonya wanamichezo hao kwa kufahamisha kuwa iwapo watakamatwa huku muda wao wa kuishi Australia umekwisha , wanatarejeshwa katika mataifa yao.Habari Zinazohusiana