Nafasi ya Uturuki barani Ulaya

Nafasi ya Uturuki barani Ulaya, Kutoka chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL anatufafanulia

Nafasi ya Uturuki barani Ulaya

Hapo awali tulishazungumzia kuwa kuongezeka kwa ubaguzi wa rangi , ufashisti, Nazism, Uislamu kwa upande mwingine kuonekana kama tishio kwa maisha yao ya tofauti, kuendelea kujifungia kwa ndani kadri siku zinavyoizidi kwenda, pia kubishana juu ya Waislamu na wahamiaji, kimsingi ni mgogoro wa kipekee barani Ulaya.Tuligusia kidogo katika makala yetu ya awali

Kutoka chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt kitengo cha cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL anatufafanulia kuhusu suala hilo ...

Hapo awali, nimefananisha mchakato wa nafasi ya Uturuki barani Ulaya, na data za Ujerumani za 28 Februari. (Http://www.star.com.tr/acik-gorus/avrupayi-28-subatindan-kim-cikaracak-haber-1168353/).

Kwa mujibu wa data hizo za wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani mnamo mwaka 2017 kuwa kulitokea mashambulizi 950 dhidi ya waislamu huku ikiwa ni mashambulizi matatu kwa siku.Hali inaonekana imeshavuka tayari mpaka huo.

Je, hii inaweza kutokana na mgogoro unaoikumba Ulaya?

Kwanza, lazima tuzingatia sababu za mgogoro huo.

“Global Uncertainity”: Mpangilio uliowekwa katika mataifa kama Marekani, Urusi, China, Uturuki, India na Latin America baada ya vita vya pili vya dunia unaonekana kuvurugika. Kutokuwa na uhakika huu kunajenga mvutano na wasiwasi katika nchi zote. Ushirika wa kiutamaduni na uadui vinaonekana kuanza tena. Kwa maana hii, mahusiano ya nchi za ndani yanafanywa upya. Badala ya kuzuia ushirikiano na ugomvi kati ya nchi, ushirikiano wa msingi unaisha.

Nchi za Magharibi haziwezi kutosheka na utandawazi: Ulaya na Marekani hazikuwa na faida ya kutosha kutoka katika utandawazi. China, India, Brazil, na nchi kama vile Uturuki, zinapata faida kubwa kutokana na mchakato huo. Kutokana na hili,nchi kama Marekani zinajaribu kutunza utandawazi wa biashara huru na kuondoa desturi amabazo zilikuwa zenye ubingwa hapo awali. Ulaya imekuwa ikichochea masuala tofauti kisiasa, kijamii, kiuchumi, kisaikolojia kutokana na kushindwa kupata  faida kubwa kutoka katika utandawazi.

Hii inaweza kueleweka kwa nchi za Magharibi. Lakini utandawazi katika nchi kama Uturuki, ambayo pia ni faida kubwa ya kuwa na wasomi na viongozi wa kisiasa, utandawazi wa zamani unaendelea je ukweli huu unatambuliwa?

Ukosefu wa historia ya pamoja ya bara  la Ulaya: Uwepo wa utofauti wa utambulisho hakato mzima wa utandawazi ni kati ya sababu kuu ya migogoro ya sasa barani humo.

Mali tofauti zilikuwa 'zinaweza kukubalika' katika nchi za mbali, ukiwa katika  nchi yako ya asili. Lakini ikija kwa jirani, mwajiri, mfanyakazi, hali hiyo ni tofauti. Kwa sababu Ulaya haina utambulisho wa aina nyingi, historia nyingi ambazo zinaweza kushinda hali hii. Uzoefu wa Ulaya wa kuishi ni tofauti kwa karne iliyopita.

 

Viongozi wasiokuwa na upeo: Vyama vya mrengo wa kushoto na mrengo wa kulia barani Ulaya, badala ya kutafuta maarifa ya kawaida dhidi ya matatzio yanayoibuka, porojo zimekuwa nyingi. Hali hii haizuii kuongezeka kwa Unazi,Ufashist.Matoeo yake siasa Ulaya zinazidi kuchafuka na ukatili kuongezeka.

 Athari za assimilation

Wale wanaohamia Ulaya kutoka katika nchi tofauti wakitaka hifadhi na kadhalika endapo watanyimnwa haki zao Ulaya au kukumbwa na matatizo basi hali hiyo itasababisha matatizo makubwa kati ya nchi walizotoka na nchi walizohamia.Hali hiyo  inalionyesha bara la Ulaya kutokuwa na uvumilivu,kuwa tishio na kuonekana kuwa nchi hizo zimejifungia kwa ndani. Mashirika ya kigaidi na vitendo vya kigaidi vinavyokuwa vikiendelea katika nchi za wahamiaji pia vinachangia katika kuvuruga mahusiano ya Ulaya na nchi hizo.

Mgogoro barani Ulaya sio mgogoro wa kutatuliwa leo wala kesho.Hii ni hatua mabayo itachukua muda mrefu mpaka hali kurudi kuwa kawaida.Wakati Ulaya wakikabiliwa na mgogoro kama hiyo ni muhimu sana kuwa na viongozi wenye busara na kuona mbali.Lakini cha kushangaza siku zinavyozidi kwenda viongozi wenye maono wanazidi kupungua Ulaya. Wataalamu, wasomi, wanaweza pia kuwa na jukumu muhimu katika kutatua hali hiyo. Kuna fikra zozote za jinsi ya kuondoakan an hali hiyo?.Haiwezekani kuwa wale wasomi wa zamani wa Ufashisti na Unazi wa Ujerumani hawayaoni maendeleo hayo.

Hata hivyo hio haitoshi kutatua mgogoro wa sasa wa Ulaya.Sauti za kutatua mgogoro huo zinazidi kupungua siku hadisiku.Vyama ambavyo vinaunga mkono ubaguzi vinazidi kuongezeka siku hadi siku.Uhuru unazidi kudidimizwa.Kiukweli sidhani kama matatizo haya yatatatuliwa ndani ya muda mfupi.Natamani isingekuwa hivyo.Watu barani Ulaya hawatokaa kulitambua hilo mpaka vita vipya vya dunia vitokee.Mustakabal wa bara la Ulaya unazidi kuingia katika kisa kinene.Sisi cha tusaidie kwa kile tutakachoweza.Tutaendelea kuzungumza kuhusu migogoro hiyo kupitia maandishi.Tutaendelea kuwaonyesha njia na suluhisho kwa kuandika tu.

Kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt,kitengo cha sayansi za siasa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL amependekeza tathmini ya mada yetu ya leo.

 Habari Zinazohusiana