Barua ya wazi kwa ubalozi wa Israel

Ahed aachwe huru, nikamatwe mimi

Barua ya wazi kwa ubalozi wa Israel

Katika usiku wa Disemba 18 kuamkia  19 mwaka 2017, jeshi la Israel lilivamia makaazi ya familia ya Ahed na kumkamata yeye pamoja na mama yake. Tangu kukamatwa kwao na jeshi la Israel, watuhumiwa hao wamekuwa wakifikishwa mahakamani mara kwa mara . Ahed Tamimi ni msichana na raia. Ahed amehukumiwa mahakamani  na hukumu ambayo ilikuwa bado haijatolewa ulimwenguni dhidi msichana mwenye umri mmdogo.

Tunatoa wito na kuomba mawakili  kutoka katika pande zote ulimwenguni, pamoja na  watetezi wa haki za binadamu na mashirika ya kutetea haki za binadamu kufanya kila liwezekanlo ili Ahed na watoto wengine wa Palestina  walindindwe dhidi ya Israel. Tulitoa wito Ahed aachwe huru bila ya ombi hilo kusikilizwa.

Na kinyume chake Ahed Tamimi amehukumiwa kifungo cha miezi  minane kutumikia kifungo. Msichana huyo aliehukumiwa na mahakama Israel ana umri mdogo ametwishwa mzigo mkubwa na jeshi la Israel.  Akiwa katika mahakama wakati wa kusikilizwa katika mahakama Ahed anonekana kuwa alikuwa katika hali isiokuwa hali ya kawaidi alipokuwa ameshikiliwa.

Tuwaache watoto huru. Msiwatumii watoto  katika mapigano na ubepari wenu. Katika kila tamaduni na imani, kuna sheria  ambazo zimepangwa kataika  vita. Katika imani zote ulimwenguni  watoto huwa wakiwekwa kando na kukingwa na athari za kivita na kulindwa kikamilifu. Tumeshuhudia kuwa watoto Israel  hawalindwi kwa kuwa  wanakamatwa na kuhukumiwa ikiwa kitendo hicho ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Nakuombeni Ahed aachwe huru  na badala yake nikamatwe mimi

Mashika ya kutetea haki za binadamu   yanataraji kuwa haki za binadamu Israel zitaheshimishwa na kuzungumzia kuhusu mashua ya Mavi Marmara ilikuwa ni kitendo ambacho kiliashiria  kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu na kupigania uhuru na sio kama inavyodaiwa kuwa harakati za kşgaidi.  Imeonekani kuwa hamtaki na hamridhishwi na uwepo wa wanaharakati wa kupigania haki za binadamu. Siwezi kupokea au kukubali jina baya  la ugaidi. Ntasimamia haki  na kupigania haki kila wakati pamoja na uhuku katika harakati.

Wito wangu kwenu upo wazi, haki ndio tunataka itendeke. Tunaomba watoto walioko katika magereza yenu kutokana na sababu za kisiasa  kuachwa huru. Ahed aachwe huru na mimi nichukue nafasi yake . Iwapo utatazama pembezuni mwenu mtaona kuwa kitendo cheno ni aibu kwa ulimwengu na cha kukemewa.

Unina imani kuwa ujumbe huu utawakera kuhusu suala hilo.

Ujumbe wangu upo wazi, mkikubaliana na hayo basi nikamatwe mimi.

Machi 21 . 2018

21.03.2018

Wakili Gülden Sönmez

Mwanaharakati wa haki za binadamuHabari Zinazohusiana