Wauza madawa ya kulevya 13 wauawa na jeshi la Polisi Ufilipino

Jeshi la Polisi nchini Ufilipino lawamalizia maisha washukiwa 13 wa biashara haramu ya madawa ya kulevya

Wauza madawa ya kulevya 13 wauawa na jeshi la Polisi Ufilipino

Washukiwa 13 wa biashara haramu ya madawa ya kulevya wauawa na jeshi la Polisi nchini Ufilipino katika operesheni ilioendeshwa  katika mkoa wa Bulacan. Jeshi la Polisi limefahamisha kuwa lilishambuliwa na walanguzi hao wa madawa ya kulenvya na polisi kujihami. Polisi walijihami kwa kufyatua risasi na kupekelea watuhumiwa hao 13 kufariki.  Tukio hilo limetokea Jumatano ambapo pia  watu wengine zaidi ya 100 wanaoshukiwa kuhusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya  walikamatwa.

Watu zaidi ya 4 000 wamekwisha uawa nchini Ufilipino wakishukiwa kuhusika na baishara ya madawa ya kulevya tangu rais Rodrigo Duterte kuchaguliwa kuwa rais wa Ufilipino. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanalaumu serikali ya Duterte yakidai kuwa inakiuka haki za binadamu.

Mkoani Bulacan, watu 32 waliuawa katika siku moja Agosti mwaka 2017 katika operesheni ya kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

 

 Habari Zinazohusiana