Uturuki yakanusha tuhuma kuwa jeshi lake limeshambulia hospitali Afrin

Jeshi la Uturuki lakanusha tuhuma dhidi yake kuwaa limeshambulia hospitali katika operesheni yake Afrini nchini Syria

afrin hastanesi.jpg

Jeshi la Uturuki limekanusha tuhuma kuwa  limeshambulia hospitali katika operesheni yake dhidi ya ugaidi Afrin nchini Syria na kusema kuwa tuhuma hizo si za kweli bali zina lengo la kutia doa baya jeshi ka Uturuki.

Jeshi la Uturuki katika operesheni yake ya Tawi la Mzaituni lilianzisha operesheni hiyo kwa lengo la kuwandoa magaidi katika mipaka yake na Syria na sio kuadhru raia.

Uturuki hukemea mashambulizi yanayowalenga raia nchini Syria.

Jambo ambalo linafahamika ni kwamba, magaidi Afrin wamechoma moto, majengo ya umma, magari, hospitali na vifaa vya matibabu kwa lengo la kulipaka matope jeshi la Uturuki katika operesheni yake dhidi ya ugaidi Afrin.

Magaidi wanatumia mbinu hiyo kutaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na kulizuia jeshi la Uturuki kuendelea na operesheni yake dhidi ya ugaidi ambapo tayari magaidi hao wamejipata katika hali ngumu wakikabiliwa na mashambulizi kutoka kwa jeshi la Uturuki na kuwaondoa katika ngome zao Afrin.

Makao makuu ya jesh i la Uturuki imesema kuwa katika siku chache zijazo wanamgambo wa PKK/PYD watakuwa wameondolea Afrin.

 

 Habari Zinazohusiana