Nauert : "Mazungumzo kati ya Uturuki na Marekani  kuhusu Manbich yaendelea"

Marekani yafahamisha kuwa mazungumzo na Uturuki ili kuafikiana kuhusu Manbich  Syria yanaendelea

Nauert : "Mazungumzo kati ya Uturuki na Marekani  kuhusu Manbich yaendelea"

Katika mkutano na waandishi wa habari , Heather Nauert amezungumzia  kuhusu hali ya Manbich na operesheni ya Tawi la Mzaituni  inayoendelea Afrin nchini Syria.

Heather Nauert amesema kuwa operesheni  ya Tawi la Mzaituni inayoendeshwa na  Uturuki  Afrin ina lengo la kuwaondoa magaidi mipakani mwa Uturuki na Syria.

Uturuki ilianzisha operesheni hiyo tangu  Januari 20 ikiwa na lengo la kuwaondoa magaidi wa PKK/KCK/PYD-YPG na wanamgambo wa  Daesh.

 Nauert amesema kuwa Marekani bado inazungumza na Uturuki kuhusu Manbich na kuwa na imani kuwa suala hilo litapatiwa jawabu.

Alipouulizwa kuhusu Afrin, Nauert alijibu kuwa sio Marekani inayoendesha operesheni katika eneo hilo.

Mmoja miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa Marekani alisema kuwa mazungumzo yaliokuwa yakitarajiwa kufanyika Machi 19 yatafanyika Machi 21.

Eneo la Manbich nchini Syria limekaliwa na magaidi wa PKK/PYD-YPG wakiungwa mkono na Marekani.


Tagi: YPG , Marekani , Uturuki

Habari Zinazohusiana