Jeshi la Uturuki laelekea mjini kati Afrin

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa jeshi la Uturuki laelekea mjini kati Afrin katika operesheni yake dhidi ya ugaidi

Jeshi la Uturuki laelekea mjini kati Afrin

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan akiwa katika mkutano wa chama cha AK mkoani mardin amesema kuwa kiwango cha magaidi wanaoangamizwa na jeshi la Uturuki katika operesheni yake ya Tawi la Mzaituni  imeongezeka na kufikia magaidi 3569.

Katika hotuba yake aliotoa, amesema kuwa  jeshi la Uturuki Jumamosi katika operesheni yake Afrin limezingira  mji wa Afrin na wanasubiri kupewa amri ya mwisho ili lianze mashambulizi ya mwisho ya kusafisha eneo hilo na magaidi.

Katika hotuba yake hiiyo alitoa Mardin rais Erdoğan amewaambia raia kuwa muda wowote wataambiwa habari njema kutoka Afrin.

Tumeshuhudia urongo ambao umegunduliwa na jeshi letu amesema rais Erdoğan  kwa ushirikiano baina ya magaidi na baadhi ya mataifa yanaodai kuwa ni washirika wetu katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Mataifa hayo yametoa usaidizi kwa maadui zetu , usaidizi wa kushangaza kwa kuchimba mahandaki ya kisasa ambayoo hata malori yanaweza kuingia.

Malori na ndege zimetoa usaidi mkubwa kwa magaidi kwa kuwafikishi asilaha ili washambulie Uturuki.

 Habari Zinazohusiana