Algeria kutuma maimamu 150 Ulaya kuongoza ibada wakati wa Ramadhani

Algeria imefahamisha kuwa itatuma maimamu 150 nchini Ufaransa kwa ajili ya kuongoza ibada katika mwenzi mtukufu wa Ramadhani

Algeria kutuma maimamu 150 Ulaya kuongoza ibada wakati wa Ramadhani

Serikali ya Algeria yafahamisha kuwa itatuma maimamu 150 nchini Ufaransa kwa ajili ya kuongoza ibada katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Taariha hiyo  kuhusu kutumwa kwa maimamu hao nchini Ufaransa ilitolewa Alkhamis na waziri anahusika na masuala ya kidini Mohamed Aissa.

Waziri huyo amefahamisha kuwa maimamu  walichaguliwa ni maimamu ambao wamehifadhi kitabu kitakatifu cha Quran na wenye uwezo wa kufikisha ujumbe  katika hutba.

Maimamu hao wanatakiwa kuwa mabalozi wa amani  na uislamu kwa kutoa hutba isiokuwa na  misimamo mikali na kuwa kueleweka.

Hayo yalifahamishwa baada ya kiongozi huyo kufanya mazungumzo na  waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gerard Collomb na waziri wa mambo ya ndani wa Algeria  Nuredine Bedui.

Maimamu 100 ndio watakaoendesha idaba  nchini Ufaransa huku wengine 50 waliobaki kupelekwa  nchini Ujerumani, Italia, Uingereza, Ubelgiji na Canada.Habari Zinazohusiana