Mwanamfalme wa Saudi Arabia amfananisha Ali Khameney na Adolf Hitler

Mwanamfalme wa Saudi Arabia asema kuwa iwapo Iran itamiliki bomu la nyuklia basi na Saudi Arabia itafanya vivyo hivyo

Mwanamfalme wa Saudi Arabia amfananisha Ali Khameney na Adolf Hitler

« Iwapo Iran  itamiliki bomu la nyuklia nasi tutafanya kama wao »

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman afahamisha katika mahojiano  aliaofanya katika kituo cha runinga cha Marekani CBS  na kusambazwa katia vituo vya runinga Saudia Arabia kuwa iwapo Iran itamiliki bomu la nyuklia basi na Saudia itafanya vivo hivyo.

Mwanamfalme huyo amesema kuwa  Saudi Arabia  itafanya haraka iwezekanavyo kuongeza juhudi katika ufundi na teknolojia kutengeneza bomu lake la nyuklia iwapo Iran itamiliki bomu la nyuklia.

Mahojiano hayo  yalipeperushwa pia katika kituo cha Al Ekhbariya na Al Arabiya Alkhamis.

Mahojiano kamili  yataoneshwa  Jumapili.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amemfananisha kiongozi wa kiroho wa Iran Ayetullah Ali Hamaney na kiongozi wa kinazi Ujerumani Adolf Hitler katika ya miaka ya 1888 na 1945.Habari Zinazohusiana