Mtazamo

ÇANAKKALE haiwezi kupitwa, UBINADAMU hauwezi kuisha. Licha ya kuwa na ufundi mdogo Jeshi la Ottoman liliweza kuilinda nchi yake kwa nguvu ya imani.

Mtazamo

Kutoka chuo kikuu cha Ankara Yildirim  Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa Dr.Kudret BÜLBÜL anatufanyia tathmini kuhusu mada yetu ya leo

ÇANAKKALE haiwezi kupitwa, UBINADAMU hauwezi kuisha

Katika historia ya nchi, kuna matukio muhimu sana yanayoathiri hatima yao. Matukio haya yanaweza kubadilisha historia wakati mwingine. Tunahitimisha miaka  103 ya vita vya Çanakkale ,vita vilivyoleta hatma ya dunia.

 Katika vita hii,  Istanbul ilivamiwa, baadhi ya sehemu za Ottoman Empire ziliachwa na kukawa na malengo ya kupeleka msaada Urusi kwa kupitia baharini.Kutokana na jambo hili nchi kama Uingereza,Ufaransa,Australia,Canada,New Zealand na India zilificha wanajeshi wake Çannakale.Kwa miaka mingi walikuwa wakijaribu kuwaondoa wanajeshi hao katika nchi.Licha ya kuwa na ufundi mdogo Jeshi la Ottoman liliweza kuilinda nchi yake kwa nguvu ya imani.

Vita vilianza Februari 1915 na kumalizika mnamo Desemba mwaka huo huo. Vita viliacha mamia ya maelfu ya watu wakiwa wamekufa,wamejeruhiwa,wamepotea na wengine kutekwa.Ilikuwa ni kati ya huzuni kubwa sana.Taa  ziliwaka. Kwa kuwa askari wengi walikuwa tayari wameuawa katika vita vya zamani, watoto wadogo walichukuliwa katika utumishi wa kijeshi katika vita hivi. Kwa sababu hii, vita hii pia inajulikana kama "vita ya wenye kumi na tano". Walikuwa wakiimbiwa"Hey vijana wenye miaka kumi na tano wanapita katika barabara za mawe.

Katika mwaka huo, vijana wengi walijiunga katika vita.Katika miji kama Galatasaray,Izmir na ambapo nilikuwa nikisomea mimi Konya ambapo shule ilikuwa imefunuliwa wakati wauatawala wa Sultan Abdulhamit I nilishindwa kuhitimu kwasababu wanafunzi walikuwa vitani.

 

Japokuwa rekodi rasmi ya vita hivyo haikupatikana lakini inakadiriwa kuwa jeshi la Ottoman lilipoteza wanajeshi elfu 250.Wengi wao walikuwa ni wasomi,waliokuwa bado wakienda chuo kikuu.Vifo vya watu wenye umuhimu mkubwa kama hao vilizua balaa.

Wanajeshi wa Ottoman waliopoteza maisha katika vita hivyo walikuwa wakitokea nchi mbalimbali kwa ajili ya kushiriki kwao kwa kujitolea.Leo pia wamebaki katika mikoa na mipaka ya Uturuki kama vile Balkan,mashariki ya kati,

Ningependa kuzungumza kuhusu yale niliyoyasikia kutoka kwa mzee wa Kosovar Eliya. Katika kijiji chake, askari wengi walijiunga na vita vya Canakkale. Lakini baada ya vita, askari wote isipokuwa watatu walifariki. Askari hao watatu walipokuwa wakirudi kijijini walichanganyikiwa ni vipi watawaambia wanakijiji wenzao kuhusu askari awale wote waliopoteza maisha katika vita.Kwasababu walijua kuwa walikuwa wakisubiriwa kwa shauku kubwa na marafiki zao,wazazi wao,watoto wao,wapenzi wao.Ingekuwa sio rahisi kuingia kwa ghafla na kuwapa habari mabya hivyo.Kutokana na hilo,kiongozi wao alitoa uamuzi na kusema askari mmoja mmoja ataenda katika kijiji hicho na sio wote kwa pamoja.Basi aliingia askar iwa kwanza na wanakijiji wote wakamfuata na kumuuliza wako wapi wengine.Alijibu kwa kusema « wanakuja,wanakuja ».Baada ya wiki moja akaingia askari wa pili na yeye alipoulizwa alijibu vivyo hivyo kuwa wanakuja.Mwanajeshi wa tatu nayeye alifuata mkondo ule ule.Hivyo ndivyo kijiji kilivyojiandaa kupatwa na huzuni na kuwa tayari kupokea habari mbaya.

Vita vya Galipoli vilikuja kama njia ya kuupinga ubeberu.Jeshi la Ottoman lilipigania hilo.Licha ya kuwa taifa la Uturuki limekuwa na teknolojia kubwa halijawahi kuuunga mkono ubeberu. Baada ya vita vya Çanakkale na baada Vita vya Uhuru nchi za Asia ya Kusini kama vile India na Afghanistan zenye Waislamu hazikuzuiliwa msaada wao. Kwa maana hii, vita vya Çanakkale ni ishara ya tumaini kwa ubinadamu.

 Leo, kuna mapigano mengi katika maeneo ya kijografia.Çanakkale ni vita vyenye hisia kali na fundisho kubwa ubepari.Hata hivyo kwas asa siasa zinazotumika ni divide and rule yani gawanya na utawale..

Kwa kweli ni vyema kupinga mashambulizi yoyote ya kibeberu. Hata hivyo, ni muhimu pia kupig mambo kama hayo.. Kwa bahati mbaya, sisi pia tunashuhudia maendeleo ya chuki / mazungumzo mengine wakati wa kukabiliana na uhasama wa leo .Chuki zimezidi.

Australia, New Zealand, nk kwa vile kulikuwa na vita vingi katika historia yao, wao pia walikaribia kuunda taifa katika vita vya Gallipoli. Hata hivyo sisi ni taifa lisilozaa chochote isipokuwa vita, ushindi, kushindwa katika historia yake. Sisi ni moja ya mataifa yasiyo ya kawaida duniani ambapo hatuna haja ya mgeni kuwa taifa na vilevile tunaweza kuwa taifa bila raia yoyote wa kigeni katika sura hii

Hii pia ni kweli kwa Çanakkale. Licha ya huzuni na majonzi mengi tuliyoyapata kutoka Çanakkale hatujatengeneza Çanakkale nyingine.Licha ya kupoteza wanajeshi 250,000,miaka kumi ya umasikini,kutengeneza mawasiliano na vilevile hasara.

Tunaangalia matukio haya kwa namna hiyo, mtazamo wa historia yetu na ustaarabu, tunakumbuka maneno ya baba wa taifa Ataturk alisema kwa Anzacs: "Kutoka mbali na nchi za mbali ni wamama ambao walituma wana na binti zao kwa machozi yako.Watoto wao wapo katika  amani na watapumzika kwa amani. Baada ya kutoa maisha yao kwa nchi hii, sasa ni watoto wetu.”

Kuzalisha hotuba ya chuki dhidi ya mashambulizi ya ki-empirealist kunatuumiza zaidi. Ndiyo ni vigumu sana. Lakini katika hali ya mashambulizi hayo, tunaposhukuru zaidi maadili ya ustaarabu wetu, na tunatumaini zaidi kwa ubinadamu. Hata kama mashambulizi ya kikabila yanafanikiwa kwa muda mfupi, ubinadamu hautaanguka na hautakuwa udhalimu ikiwa tuna njia isiyozalisha mambo hayo. Jitihada za kikoloni zinazozingatia riba, unyonyaji zote zitapotea na kuanguka baadae.

Kutoka chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt kitengo cha Sayansi za Siasa Profesa. Dr. Kudret BÜLBÜL alipendekeza tathmini ya suala hilo

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 Habari Zinazohusiana