Ulimwengu washuhudia mauaji Ghuta

Kipiindi chetu cha leo kimetaarishwa na Yazar Can ACUN kutoka katika  shirika la utafiti wa sisasa, uchumi na jamii

Ulimwengu washuhudia mauaji Ghuta

Katika  mji mkuu wa Syria Damasko, eneo la Cobar Ghuta Mashariki   na maeneo mengine ambayo karibu mji mkuu yamekaliwa na jeshi la Assad na makundi ya waasi yanayounga mkono  serikali ya Assad  tangu kwama 2013. Maeneo hayo yemakliwa na  waasi hao kwa kipindi cha zaidi ya  zaidi ya miaka mitano tangu mwaka  2013.

Eneo la Ghuta Mashariki  ni eneo ambalo kwa sasa  katika kipindi kirefu limeshambuliwa na jeshi la Assad na jeshi la anga la Urusi.

Kitika kipindi cha siku 3  kuliendeshwa mashambulizi ambayo yalipelekea watu zaidi ya 250 waliuawa. Kutokana na tukio hilo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha mkutano na kufikia hatua ambayo ilipelekea kusitishwa kwa mapigano.

Uamuzi wa Umoja wa Mataifa kusitisha mapigano  Ghuta Mashariki na kuzuia mauaji  ndio ilikuwa lengo la mkutano huo kuandaliwa.

Mashambulizi ambayo yanashuhudiwa Ghuta ni wazi kuwa yanaelenga hospitali, shule na waathirika wa kwanza katika mstari wa kwanza ni watoto na wanawake. Hali hiyo inazidisha ugumu ya kufikisha misaada katika eneo hilo.

Kipiindi chetu cha leo kimetaarishwa na Yazar Can ACUN kutoka katika  shirika la utafiti wa sisasa, uchumi na jamii.

Baada ya  kufunguliwa kwa maeneo matatu ya ulinzi kutokana na mkutano wa Astana  tumeshuhudia ongezeko la mgogoro. Katika eneo la Humus, Guta na Dera  kulitakiwa pia kuwekwa ulinzi  baada ya mazungumzo ya Astana.  Katika mapigano ya Idlib , serikali ya Assad kwa ushirikiano na makundi ya waasi yanayomuunga mkono  yalihamia Ghuta na kuanzisha mashambulizi makubwa.

Kabla ya kuanza kwa operesheni ya ardhini, eneo la Ghuta Mashatiki lilikuwa likishambuliwa na jeshi la serikali na jeshi la anga Urusi.

Jeshi la seriakli ya Assad linashambulia bila ya kujali  raia  na kuwaweka pamoja  na waasi wanaolengwa  na jeshi  serikali . mfumo unaototumiwa haujali  anelengwa na kuharibu kil akitu baada ya masahmbulizi. Mashambulizi hayo hutekelezwa kwa ushirikiano bain aya jeshi la Urusi na Syria.

Kulingana na mkakati  huo, au hali hiyo  baraza la  usalama la Umoja wa Mataifa  lilikutana  na kujadili hali inayoendelea nchini Syria na kujaribu kupatia suluhu mgogoro wa Ghuta Mashariki.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa  lilitangaza uamuzi wa kusiiitishwa kwa mapigano  , uamuzi ambao ulikuwa chini ya vitisho vya kura ya turufu ya Urusi. Mapambano dhidi ya kundi la kşgaidi la Daesh alivyokuwa dhidi ya kundi la al Qaida na makubaliano ya baraza la Umoja wa Mataifa.

Rasmi operesheni za jeshi la Urusi Syria ni kupambana na kundi la  wanamgambo wa Daesh na kundi la kigaidi la al Qaida. Ila ukweli halisi ni kwamba upinzani wa msimamo wa wastani Syria dhidi ya serikali ndio  unaolengwa katika mashambulizi ya kikjeshi  bila ya kutofautisha raia na makundi ya wapiganaji.

Kwa upande mwingine  kutokana na kwamba hakuna  mikakati ilioandaliwa iwapo mikataba na makubaliaona yatakapovunjwa ni adhabu au vikwazo aina gani vinatakiwa kuchukuliwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Mashariki mwa Ghuta , maeneo kama  Ahrar uş Şam na makundi kama  Ceys el İslam ni makundi ambayo yaliwekwa nje ya makubaliano ya kusitisha mapigano.  Jambo hilo lilinukuliwa kimakosa baada ya uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu  usitishwaji wa mapigano.

Mapigano huzka mara kwa mara bain aya  makundi hayo  Ghuta Masahriki na kupelekea watu wengi  kuzuiliwa. Operesheni kali ziliendeshwa  dhidi ya makundi kadhaa  katika eneo la İdlib wakati ambapo Urusi ilikuwa ikizungumza kuhusu kusitishwa kwa mapigano.

Ni wazi kuwa mashambulizi ya anga yanayoendeshwa kwa ushirikiano bain aya  jeshi la Assad na lile la Urusi , mashambulizi hayo ni uuaji  na ukatili amboa unastahili kukemewa vikali Ghuta. Ghuta Mashariki maelfu ya raia  ambao wamezuiliwa  wapo mstari wa mbele kupoteza maisha wakati  wa mashambulizi.

Baada ya  mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuliafikiwa kusitishwa kwa mapigano  kuanzia majira ya asubuhi  saa tatu hadi mchana saa nane. Maafikiano hayo ya kusitisha mapigano ni kwa lengo la kuhakikisha kuwa misaada ya kiutu inaingia Ghuta kwa manufaa ya raia wenye kuhitaji misaada.

Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yalivunjwa na vikosi vya Assad na makundi ya wapigani wanaouunga mkono serikali siku ya kwanza kwa kushambulia Ghuta Mashariki.  Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na   kitengo cha usalama na ulinzi Ghuta, Ghuta ilishambuliwa katika wakati ambao ulisainiwa kuwa ni wakati wa kusitisha mapigano na  kama iliovyoafikiwa  .

Serikali imeandaa silaha zake  kwa jambo lolote ambalo linaweza kutokea.

Uturuki moja ya mataifa amboya yalipendekeza  mazungumzo ya Astana ili kusitisha mapigano Ghuta Mashariki  inafanya kila liwezekanalo  kufikia katika lengo hilo.Habari Zinazohusiana