Wanamgambo 400 wa kundi la Daesh wakamatwa na jeshi huru la Syria İdlib

Jeshi huru la Syria lawakamata wanamgambo 400 wa kundi la kigaidi la Daesh katika operesheni yake İdlib

Wanamgambo 400 wa kundi la Daesh wakamatwa na jeshi huru la Syria İdlib

Jeshi huru la upinzani la Syria lafahamisha kuwakamata wanamgambo 400 wa kundi la kigaidi la Daesh katika opereshni yake iliondeshwa İdlib nchini Syria.

Wanamgambo hao wamekamatwa Jumanne wakijaribu  kungia katika eneo la İdlib  Kaskazini-Magharibi mwa Syria.

Taarifa zilizotolewa na mwanahabari wa kituo cha Anadolu zimefahamisha kuwa  ushirikiona baina ya makundi ya upünzani imefaanikisha zoezi hilo ambalo limetambulishwa kuwa kitendo cha kishujaa.

Katika operesheni hiyo  wanamgambo wengine zaidi ya 10 wameripotiwa kuuawa.

 

 


Tagi: Syria , İdlib , ugaidi , Daesh

Habari Zinazohusiana