Mtazamo

Waturuki wa Thrace ya Magharibi : Kutokubalika kwa Waturuki

Mtazamo

Waturuki wa Thrace ya Magharibi : Kutokubalika kwa Waturuki

 

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa Dr.Kudret BÜLBÜL anafanya tathmini ya mada ya leo

Fikiria kwa muda kama wewe hujitambulisha mwenyewe kwa kutumia  (Kijerumani, Kiarabu, Kituruki, Muislamu, Mkristo, mpagani...) na ndani ya nchi yako unayoishi zaidi ya maelfu ya miaka , watu bado hukuambia "wewe sio yule" na "jumuiya yako haipo katika hii nchi"

"Unajishughulishaje na mataifa ambapo watu hujitambulisha wenyewe?. Ni katika nchi tu kwamba kukubali na kuiheshimu ni suala la jinsi jumuiya zinavyojitambulisha wenyewe. Inawezekana ukasema hakuna kitu kama hicho zama hizi.

Wewe unaweza kuwa sawwa kusema kuwa jambo kama hili halipo tena katika jamii na nachi zetu za leo kutokana na uelewa wako lakini kwa bahati mbaya jambo hili linazidi kuendelea mpaka hivi sasa."

 Hii bado inatokea Ugiriki, nchi ya Umoja wa Ulaya. Watu wamekuwa wakijitahidi kuzungumza Kigiriki na kuwaWagiriki kwa zaidi ya maelfu ya miaka ili kujitambulisha kama wao ni wakazi wa hapo licha ya kuwa na utambulisho wao wenyewe wa Kiislam na Kituruki.

Nazungumzia waturuki wa Thrace magharibi.Waturuki wa Magharibi ya Thrace walikuwa wakiishi katika nchi hizo kabla hata ya utawala wa Ottoman. Hata baada ya kuanguka kwa utawala wa Ottoman idadi ndogo ya waturuki waislamu waliokuwa wakishi Ugiriki ilipewa haki zao na jumuiya ya kimataifa.Lakini cha kusikitsha ni kwamba haki hizo zipo katika maandishi tu na sio utekelezaji.. Leo, ntazungumzia aina tat uza ukiukwaji wa haki hizo

Mtu aliyejeruhiwa

Haki zote na uhuru kama vile haki za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni ni muhimu na vilevile ni  mojawapo ya haki za msingi za kibinadamu ambazo mtu atatumia kujitambulisha mwenyewe . Ni haki ya ontolojia. Kwa mujibu wa Kifungu cha 6 cha Azimio la Umoja wa Haki za Binadamu, "Kila mtu ana haki ya kutambuliwa kihalali popote alipo". Uwepo wa mtu unajitambulisha wenyewe kwa sehemu aliyopo. Kukataa utambulisho wa mtu au mali ni sawa na kukataa kuwepo kwa mtu huyo. Pengine hii ndiyo sababu Emile Maalouf katika kitabu chake cha  "Deadly Identities" alibainisha kuwa utambulisho wa mtu unapatikana pale alipojeruhiwa. Wakristo wa kwanza na Waislamu wa kwanza, walifanya mapambano dhidi ukandamizaji, mateso na kuvumilia suala zima la utambulisho.Huo ni mfano halisi.

Utambulisho wa Kituruki uliokataliwa

Wale wanaoishi katika mazingira ya kutotambuliwa kama waturuki katika Thrace ya Magharibi sio tofauti na tunachozungumzia. “Umoja wa waturuki Xanthi “ulianzishwa mwaka wa 1927 na uliendelea kuwepo mpaka miaka ya 1980. Mnamo mwaka wa 1983, ishara ya jina "Türk" ilitolewa na vikosi vya usalama. Shughuli zao haziruhusiwi. Shirika hilo limefungwa na Mahakama za Mitaa za Kigiriki na Mahakama ya Cassation kwa sababu "hakuna Mturuki katika Thrace ya Magharibi".

Waturuki wa Kiislamu wa Thrace Magharibi kisha wakaenda kwa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu. ECHR ikauona umoja wa waturuki Xanthi kuwa sahihi mwaka 2008. Lakini kulingana na sheria ya Kiyunani, uamuzi wa ECHR hautoi matokeo ya moja kwa moja. Ni muhimu kufanya maombi kwa mara nyingine.

Jamii wa waturuki nchini Ugiriki wamekuwa wakijitahidi kwa miaka kumi iliyopita kutekeleza uamuzi wa ECHR wa Ugiriki. Kesi ya mwisho inayohusiana na hili ilisikilizwa tarehe 9 Februari 2018 katika Mahakama ya Rufaa ya Komotini, na hakuna matokeo yaliyotokea.

Imekuwa miaka 35 kamili ya mapambano ya marekebisho ya maombi ambayo yalianza mwaka 1983 na kukiukwa kwa haki ya msingi ya kibinadamu.Waislamu wa magharibi mwa Thrace waliendelea na mapambano yao bila kuacha sheria. Wamekuwa wanasubiri haki kutoka Umoja wa Ulaya, ambayo haijawahi kushinikizwa na Ugiriki kwa miaka 35. Lakini katika mchakato huu, Jimbo la Kigiriki linalenga umuhimu kwa sera za vitisho badala ya haki.

Siku ya kitaifa ya Upinzani

Januari 29, 1988 waturuki wa magharibi mwa Thrace, walijipanga kupinga kuandamana dhidi ya uamuzi wa mahakama ya Ugiriki kuhusu kuwanyima haki zao wao kama waturuki. Baada ya siku hiyo ilitangazwa kuwa Januari 29 ni "National Resistance Day". Lakini Ugiriki hupendelea njia ya kukandamiza na kuzuia shughuli katika siku hiyo.

Siku ya kitaifa ya Upinzani mwaka 1990, licha ya jitihada zote za kuizuia maelfu ya watu walishiriki kujitambulisha. Lakini wakati wa maandamano haya ya kidemokrasia na ya halali, Wagiriki fanatic waliwashambulia Waturuki. Kwa siku mbili,mali za waturuki waislamu wa mahala hapo zilikuwa zikiharibiwa na kuteketezwa.  Mufti Mehmet Emin Aga na Ahmet Turk ni kati ya waliojeruhiwa wakati wa maandamano hayo na polisi wa Ugiriki walionekana kufumbia macho suala hilo.

Je ni utambulisho wa Kituruki tu ndio unaokataliwa?

Kwa bahati mbaya, matatizo ya Ugiriki hayakuanza tu kwa kukataa utambulisho wa Kituruki peke yake. Ingawa wanahakikishiwa na sheria na makubaliano ya pamoja, hawaruhusiwi kuchagua viongozi wao wa dini wenyewe.Hivi ni vikwazo juu ya ibada  ya mtu.

Wale wanaojiuliza kuhusu matatizo ya Waturuki wa Thrace ya Magharibi T wanaweza kuangalia Ripoti ya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Katip Çelebi kwa Kituruki, Kigiriki na Kiingereza.

Ukiukwaji katika kanisa la Akdamar wakati wa kufungua ibada, Mor Gabriel kurudi nchi ya makao ya watawa,  elimu ya Gokceada katika shule ya Ugiriki inayogharamiwa na waturuki na marejesho ya kanisa la wabulgaria Istanbul ni hatua nzuri katika kutekeleza sera ya kutosha ili kuzuia ukiukwaji huo amabo umefanyika ndani ya miongo kadhaa na ilifanywa na taasisi za EU na taasisi na mashirika ya kimataifa.

 

Ukiukwaji huu ni wa kusikitisha katika ulimwengu wa kiislamu,mashirika ya haki za binadamu na wasomi nchini Uturuki, wakati wakiwa na maarifa makubwa sana na maslahi kuhusiana na masuala ya kawaida ya haki za binadamu katika nchi yao wenyewe, Ugiriki ambayo ni jirani.Sisi wengi hufanyia kazi ripoti ya Ukiukaji wa Haki za Binadamu, tuna ujuzi zaidi kuhusu ukiukwaji dhidi ya watu wetu katika nchi nyingine.

 

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa,suala hili limefanyiwa tathmini…

Kwa wale wote wanaojiuliza kuhusu matatizo hayo  ripoti imeandaliwa kwa kiingereza na kigiriki katika chuo kikuu cha Celebi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu .Ripoti hio imezungumzia ufunguzi na kurejeshwa kwa kanisa şa Purple Gabriel,elimu ya kituruki katika shule za Ugiriki,muelekeo mwingine kama vile kanisa la Bulgaria mjini Istanbul na  kuchukuliwa kwa hatua nzuri kama kuitikiwa kwa mashtaka ya waturuki katika taasisi na mashirika ya EU ili kuzuia ukiukwaji kwa miongo kadhaa inayokuja.

Na ukiukaji huu ni wa kusikitisha kwa ulimwengu wa Kiislamu, mashirika ya haki za binadamu na wasomi nchini Uturuki, wakati wakiwa na maarifa makubwa sana na maslahi kuhusiana na masuala ya kawaida ya haki za binadamu katika nchi zao wenyewe.Sisi wengi hufanya kazi kama kuripoti Ukiukaji wa Haki za Binadamu, tuna ujuzi zaidi kuhusu suala hilo.

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit katika kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL alipendekeza tathmini ya suala hilo.Habari Zinazohusiana