Mtazamo

Je mambo yanayozidi kuisambaratisha dunia,yataendelea kufanywa mpaka lini?

Mtazamo

Je mambo yanayozidi kuisambaratisha dunia,yataendelea kufanywa mpaka lini?

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha sayansi za siasa Dr. Kudret BÜLBÜL anatoa tahthimini kuhusu kuhusu suala hilo.

Tunapotazama matukio kabla ya Vita vya kwanza vya dunia ,ikiwa ishara na mifano hai haichukuliwi basi hio tunaiita “kujirudia kwa historia”.

 Kabla ya kubadilika kwa karne, ilikuwa karibu kama utambulisho mpya, mambo mapya vilikuwa vikiipigania dunia. Vita dhidi ya wafalme vilitangazwa katika kila kona ya dunia. Kutoka kila jiografia, wengi wasio na chimbuko, wapya, wasiojulikana, watu wapya waliongezeka. Matokeo yake, kwa kipindi fulani, utawala wote, ikiwa ni pamoja na Ottoman, Uingereza, Austria Hungary, ulitawanyika.

Kwa bahati mbaya ulimwengu hauwezi kuondokana na mapinduzi ya Kifaransa na utaifa wake. Wimbi hili linaendelea kusambaza sumu duniani kote. Vita vya II vya dunia pia havikutosheleza kwa wimbi hilo kusimama.Utaifa uko palepale,mwendo ni ule ule.

Tukitizama hali yetu ya sasa,mambo yanaonekana kuwa yaleyale kabla ya vita vya kwanza vya dunia.

Balkans, Ulaya ya Mashariki, Mashariki ya Kati, Hispania vinaelekea kuteketea.

Siyo tu mataifa ambayo yamevunjwa ,mengine yapo njiani kuangamia. Uharibifu uliotengenezwa, atomic ,sehemu zote zimefanywa kuwa za kulipuka saa yoyote.

Kutokana na mambo hayo mapya ulimwengu haujapata amani katika zam aza utawala wa Dola. Kinyume chake, ulimwengu umegawanyika zaidi, nchi zote zipo hatarini kuangamizwa.

 

Mambo yanayoiangamiza dunia yataendelea kufanywa mpaka lini? Ukabila utaachwa wapi?

Kwa kweli, hii siyo hali ambayo watu hawajui. Wakati wa kipindi cha Ukabaila (feudalism)Ulaya, hali ya mtu aliyefungwa / mtumwa, kununuliwa na kuuzwa kwa ardhi inajulikana.

Watu walikuwa na uhuru kiasi gani katika zama kabla ya utawala wa Ottoman?

Mgawanyiko wa nchi na binadamu vinafanya vipi ugumu katika uchumi, biashara, afya, elimu, usafiri, na maisha ya kila siku?

Mgawanyiko huo na kutawanyika kwa jamii tofauti kunapelekea madhara mengi.Watu wanabaki wakiwa peke yao.

Hii itasababisha matatizo mengi ya kisaikolojia, kijamii na patholojia pamoja na matatizo makubwa ya usalama. Leo, mitandao ya uhalifu au mashirika ya kigaidi ambayo mataifa yote yanapata shida kukabiliana nayo ,zaidi ni mashirika ya kigaidi yaliyo na watu mmoja au vikundi vidogo. Ni nini kinachoweza kuwa hatari zaidi kuliko kuharibiwa utambulisho wake mtu,kujitenga na kuwa na maadili yasiyokuwa sawa. Au kikundi kidogo cha watu ambao wamejijengea thamaniyao wenyewe.

Mpaka lini ulimwengu utaendelea kuangamia kutokana na mambo haya? Mataifa yanazidi kuangamia kutokana na ukabila ,ubaguzi wa rangi na vitu kama hivyo.

Nim paka lini mtindo wa “divide and rule” yani kwanza tenganisha na kisha tawala,utaendelea?

Ukabila na maadili yanayoendelea sio sawa na si busara kwa binadamu wala uislamu.

Katika hali hiyo hatuwezi kusema kama Necip Fazıl,kuwa "subirini,njia hii ni ndogo kwa umati wa watu kupita,mikono yangu wazi kama mkasi".

 Kwa binadamu, tunahitaji kuendeleza hali ya hewa, maoni, maono ambayo hayatagawanyisha bali kuunganisha zaidi. Tunahitaji kugawana zaidi, sio ubinafsi, ushirikiano zaidi, mtazamo wa maadili, kanuni, haki. Tunapaswa kuwa na malengo zaidi ya kuishi pamoja kwa amani, amani na ulimwengu wote, wanadamu, maadili, maadili ya Kiislamu (ambayo mara nyingi yanaingiliana). Tunapaswa kuendeleza sera katika mwelekeo huu.

Lakini tutafanya hayo yote kwa njia ipi?

Ki ukweli ni kwamba majibu tunayo lakini ni vigumu kutekeleza. Ni vyema kuwa na uvumilivu.

Kwanza, nchi zote zinapaswa kutekeleza sera za kuzuia zaidi makundi tofauti ya kikabila, kiitikadi, makundi ya kidini yakiwa peke yake. Ikiwa wanaangalia, wanapaswa kusisitiza juu ya siasa hizi, kupuuza mifano ya uwongo na hukumu. Uumbaji wa Yunus Dervish ni wa kuvumiliwa kwa sababu ya Muumba.

Aina hii ya sera inaweza kufuatwa lakini haitoshi. Kwa sababu hii, muhimu zaidi ni: haki za binadamu, haki za msingi na uhuru havipaswi kutumika kama njia ya sera za kigeni. Nchi hazipaswi kuharibiwa kwa njia moja ama nyingine. Tofauti kati ya nchi na nchi au ndanş ya nchi yenyewe hazipaswi kutumika kuziangamiza nchi hizo.

Nchi ambazo zina utambulisho na tamaduni ndani yake zinapaswa kuwa makini sana dhidi ya madhumuni hayo ya watendaji wa kifalme. Hazipashiwi kushinikiza watu wake wenyewe katika mikono ya watendaji wasio na haki.

Wale wanaofikiri kuwa utendaji huo wa kşmataifa ni sawa,je hatupaswi kuwa na wito kuhusu hali halisi ya siasa kwa dunia ya leo?.Je hatupasw, kuwahimiza wanadamu kufanya vitu vya manufaa kwa binadamu wote?.

Hata kama uchumi ndio kila kitu katika maamuzi tofauti,tunapaswa kufahamu kuwa kila sehemu ni muhimu ulimwenguni iwe ndani au nje ya nchi.

Hata kama itachukua muda mrefu,lakini siku zote wema hushinda.

 

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha Sayansi ya Siasa Profesa. Dr. Kudret BÜLBÜL alipendekeza tathmini ya suala hilo ...Habari Zinazohusiana