Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Hitoria ya kuliunganisha bara la Afrika,jitihada za Kwame Nkrumah,Muammar Gadaffi na Paul Kagame

Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Katika historia ya hivi karibuni ya Afrika, Muungano wa Afrika “Pan Africanism” umepitia vipindi viwili muhimu vya mawazo.

Katika miaka ya 1960, miaka ambapo nchi za Kiafrika zilipata uhuru ndio ulikuwa wakati ambapo muungano wa Afrika ulikuwa na nguvu. Hata hivyo, kumekuwa na makubaliano kati ya viongozi wa nchi mpya zilizojitegemea juu ya jinsi Afrika yenye umoja itakavyoundwa.

Baadhi ya viongozi waliutetea muungano waAfrika na kushauri  uundwe haraka iwezekanavyo, huku wengine walisema kwamba muungano huo unapaswa kuundwa taratibu ndani ya muda mrefu. Hatua ambapo pande mbili zingejiunga pamoja na kuwa Afrika  huru na yenye kufanya kazi kwa ushirikiano.

Baada ya mazungumzo magumu na majadiliano kati ya pande hizo mbili, ushirikiano wa taratibu ulikubaliwa na Shirika la Umoja wa Afrika lilianzishwa tarehe 25 Mei 1963,ambapo ilipiganiwa kuunganishwa kwa bara chini ya juhudi za Rais wa kwanza wa Ghana Kwame Nkrumah.Juhudi hizo, mpaka leo zimekuwa ni moja ya alama muhimu zaidi kwa muungano wa Afrika.Jina la Kwame Nkrumah ni jina muhimu katika historia ya kutaka kuliunga bara la Afrika.

Mabadiliko katika siasa za dunia baada ya Vita vya baridi pia yalionekana katika bara la Afrika. Sasa Shirika la Umoja wa Afrika limeanza kushindwa kukabiliana na matatizo mapya ya bara.

Ndiyo maana mwishoni mwa miaka ya 1990 juhudi zilianza kutekeleza mageuzi ambayo shirika lilihitaji. Kama matokeo ya mageuzi haya, mwezi Julai 2001, Muungano wa Afrika ulianzishwa badala ya Umoja wa Afrika. Katika miaka ya 1960 kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Afrika kulihamasishwa sana na Kwame Nkrumah kama vile Muammar Gadaffi ,kiongozi wa zamani wa Libya alivyolichukua jukumu hilo.

Gaddafi alionekana kama kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika kati ya watu wa Afrika kwa sababu ya juhudi zake za kuanzisha muungano wa Afrika. Hata hivyo, kama vile Nkrumah alivyoshutumiwa na Marekani kuwa na nia ya kufikia malengo yake ya kisiasa ndivyo Gaddafi alivyoshtakiwa.

Mawazo ya Gaddafi yalifanana sana na mawazo ya Nkrumah na ndio sababu ya Gadaffi kufanya uwekezaji mkubwa katika nchi za Afrika na kuonekana shujaa katika macho ya watu wa Afrika sababu iliyozifanya nchi za magharibi kuupinga vilivyo uongozi wake.

Wakati matukio yalipoanza Libya mwaka 2011, nafasi ya Gadaffi Umoja wa Afrika ilibadilika.

Mchango wa Gaddafi kwa Umoja wa Afrika ulikuwa ni mkubwa sana. Pia kifo cha Gadaff kilisababisha pengo katika Umoja wa Afrika.

Katika miaka michache iliyopita, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameanza kuonekana kama kiongozi ambaye atajaza nafasi iliyoachwa na Gaddafi na ameanza kufanya jukumu muhimu katika Umoja wa Afrika.

Paul Kagame, aliyeonekana kuwa  sura mpya ya Afrika, anaonekana  kujaribu kuujenga muungano wa Afrika kwa kutumia uchumi, tofauti na viongozi wa zamani.

Tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, malengo ya kisiasa yamekuwa yakiharibiwa.

Kagame ana jukumu muhimu katika mageuzi yaliyoanzishwa kubadilisha Umoja wa Afrika katika mfumo wa kisiasa ambao utakidhi mahitaji ya kiuchumi ya watu wa bara la Afrika. Katika Mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Kigali Julai 2016, Paul Kagame alipewa nafasi ya kuongoza juhudi za mageuzi ya Umoja wa Afrika.

Kagame ametengeneza kamati ya watu wataalamu tisa  akiwemo rais wa zamani  wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Donald Kaberuka, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika Carlos Lopes na Mwanauchumi Acha Leke.

Kazi ya Tume ni kutoa pendekezo la marekebisho ambalo shirika linahitaji ,katika mkutano mkuu.

Lengi ni kuimarisha sehemu ya harakati ya mageuzi ya Umoja wa Afrika iliyopangwa katika maeneo matatu.

Shirika linatengeneza mfumo ambapo Afrika itaweza kusikika duniani na marekebisho kufanywa katika amani ya bara, usalama, ushirikiano wa kiuchumi na vilevile mageuzi katika siasa.

 Jambo la pili ni kupunguza mzigo wa Umoja wa Afrika kushiriki katika mashirika na taasisi nyingine za kikanda.

Tatu, udhamini wa Shirika unafanywa na nchi mwanachama kwa asilimia  0.2% ya kodi kutoka katika baadhi ya bidhaa kwenye shirika la biashara duniani.Ufadhili wa zaidi ya asilimia 80 ya marekebisho hayo umefanywa na Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na washirika wa kigeni,hali itakayoisaidia Afrika kujitegemea.

Endapo lengo litafikiwa, basi hatua muhimu kuelekea lengo la 2063 la Muungano wa Afrika itachukuliwa.

Mkutano wa 30 wa Umoja wa Afrika, ulifanyika mjini Addis Abeba, mji mkuu wa Ethiopia kati ya tarehe 28-29 Januari.Mkutano huo ulikuwa ni muhimu.

Kwani kwa mara ya kwanza, Rwanda ilichukua uongozi wa Umoja wa Afrika. Inatarajiwa kwamba Paul Kagame atatoa mchango mkubwa katika kuimarisha Umoja huo. Kuna sababu nyingi za kufikiria hivyo:

 Kati ya viongozi wa Afrika, Kagame anajulikana kwa kuwa na nidhamu katika kazi. Kwa kuongeza, Paul Kagame ameonyesha uongozi wa mafanikio katika bara zima kwa kuifanya Rwanda kuwa mfano wa Afrika ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Muhimu zaidi ni kuwa Paul Kagame ni tofauti na kiongozi wa Afrika, ana hamu ya kuhamisha mafanikio yake katika nchi yake ,Umoja wa Afrika.

Pia fikra za Kagame  kuhusu muungano wa Afrika zimeanza kupata nguvu na kusikilizwa katika Umoja wa Afrika na watu wote Afrika kwa ujumla. Kutokana na viongozi tofauti wa Afrika kutaka kujitegemea na kupunguza kutegemea nchi za nje,mawazo ya Paul Kagame yanatiliwa maanani.

Kwa mfano, nchi karibu 20 zimeanza kutekeleza mfumo wa kodi wa 0.2% .

Lakini Umoja wa Mataifa utalazimika kutumia nguvu nyingi katika kutatua migogoro inayolikumba bara hilo.

Hakika katika miaka ya hivi karibuni,imekuwa ni jambo la muhimu kwa Umoja wa Afrika kutatua majanga barani Afrika.

Paul Kagame, atatumia nguvu nyingi katika kutatua migogoro ya Afrika na kutimiza ndoto ya kuwa na Afrika iliyo moja.Katika mkutano uliofanyika,viongozi wengi walidai kuwa mategemeo ya muungano huo ni makubwa kutokana na kuwa na kiongozi muadilifu kama Paul Kagame.

Paul Kagame ni kati ya majina yatakayokumbukwa katika historia ya bara la Afrika kama vile alivyo Muammer Gadafi na Kwame Nkrumah.Habari Zinazohusiana