Mtazamo

Je, ninawezaje kutatua tatizo la utendaji wa watendaji wa kimataifa?

Mtazamo

 

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim  Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL amefanya tathmini kuhusu suala hilo.

Tulizungumzia kwa ufupi wiki iliyopita kwamba migogoro ya kikanda haiwezi kutatuliwa na watendaji wa kimataifa. Leo nataka kuelezea zaidi kuhusu somo hili.

Tunawasiliana na Dr.Kudret BÜLBÜL kutoka chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa, kuwasilisha tathmini yake kuhusu suala hilo ...

Hivi karibuni, kumekuwa hakuna utulivu katika mataifa yaliyoingiliwa na uongozi wa watendaji wa kimataifa au watendaji . Kinyume chake, inaweza kusemwa kuwa utulivu unapatikana katika mataifa yasiyokuwa na watendaji hao. Mara nyingi nchi hizi zinakabiliwa na vifo vingi, machozi, uhamiaji mkubwa, migogoro ya kiuchumi, na inakuwa ni vigumu kuishi.

Tukiangalia kwa haraka matatizo ambayo watendaji wa kimataifa wamehusika kikamilifu katika kipindi cha hivi karibuni ,tutaona ukweli ambao ni mchungu.

Umoja wa Sovieti ulihusishwa lakini Mgogoro wa Afghanistan, ambao ulianza na kuingia kwa USSR, bado unaendelea, licha ya maumivu ya muda mrefu.

Ndiyo, Saddam alikuwa dikteta. Chini ya utawala wa kibabe wa Saddam, kulikuwa na malalamiko makubwa sana. Lakini baada ya kuona kile kilichotokea Iraq na kuingilia kati kwa watendaji wa kimataifa, Wairaq wangapi wangependelea Iraq ya leo na sio Iraq ya Saddam?

Kuna tumaini kiasi gani Walibya wanayo kuhusu siku zijazo za Libya,hasa baada ya kuingilia kati kwa watendaji wa kimataifa?

Na Syria?.Kumekuwa na mauaji ya mamia ya maelfu ya watu katika miji kama vile Damascus, Aleppo, ambapo sasa ni vigumu kutabiri maisha ya baadae ya Syria hasa ambapo watendaji wa kimataifa hawatambuliki tena.

Pakistani, ambayo imekuwa ikipata cha moto  kwa miongo kadhaa nchini Afghanistan, na hizi sasa ni mgogoro mkubwa zaidi kuliko miaka iliyopita, na inapata vitisho kutoka Marekani.

Amani gani ililetwa na Dayton kwa waislamu wa Bosnia? Ambapo kiongozi mahiri kama Aliya alilazimika kusaini mikataba ya vitisho,usaliti na ahadi zisizokuwa za kweli?.Huku wabosnia wengi wakiwa wamelala katika makaburi yao,wauaji wa serbia wamekutwa na hatia na mahakama ya kimataifa lakini huo huo nchi imevunjwa kuwa Bosnia na Herzegowina, Waserbia, Wakroatia na Bosniaks .Nchi imekosa nguvu.

Tukitizama Myanmar,na waislamu wa Rakhine,makazi yao yalichomwa moto na wananchi kuuawa hali iliyofanya kuwe na wahamiaji wa kulazimishwa kutoka Rohingya / Arakan na kukimbilia nchini Bangladesh.Wamekuwa wakienda Bangladesh kwasababu umbali wa kuja Ulaya na nchi za magharib ni mkubwa.Haijulikani kama watendaji wa kimataifa watawapatia watu hawa suluhisho kwani jambo hilo linaweza kuwa halina maslahi kwao.  

Hatua ambapo Palestina imefikia kutokana na hatua za watendaji wa kimataifa katika karne iliyopita ni mbaya. Wapalestina wanaishi katika uvamizi wa Israel na sehemu ya kuishi ya wapalestina inapungua siku hadi siku kutokana na uvamizi wa Israel.

Mifano ya suala hili ni mingi sana.

Kwa bahati mbaya, matatizo yote yaliyotajwa hapo juu ni mgogoro unaohusika na wasomi wa kijiografia. Hali hii pia inahitaji kuelezwa na kutathmini.

Kwa nini matatizo yanazidi pale watendaji wa kimataifa wanapoigilia kati?

Labda sababu ya msingi ya hii ni mawazo ambayo watendaji wa kimataifa wanayo. Kanuni ya siasa za kimataifa ni kwamba hawajali haki bali wanatizama maslahi. Mwakilishi wa Uturuki EU , Katie Pirie alisema wiki hii kuwa  muuaji wa watu elfu 40 amesema kuwa kundi la kigaidi PKK ni tishio kwao wenyewe na huo ni mtazamo. Mtazamo huo hauleti wasiwasi kwa wanadamu ambao hawajapata  shida yoyote, mpaka pale shambulizi litakapofanywa kwao.

Mbinu hii haijulikani na wengi. Hatuwezi kuangalia tatizo lolote na mtazamo wa namna hii,mtazamo wa mfumo wa kibeberu. Hatuwezi kujitizama wenyewe tukifanya udanganyifu, bila ya  kuwepo kanuni yoyote. Katika ustaarabu wetu pia kuna sheria ya vita. Tuna mtazamo ambao sio tu hufanya kuwa chombo cha vita vya kisheria, lakini pia mfumo wa kisheria wa vita, lakini vita hivyo ni vya halali.

Ni wazi kuwa watendaji wa kimataifa hawaoni thamani ya haki na hufanya lolote kufikia malengo yao, matatizo ya hapo awali tuliyoyaelezea hayawezi kutatuliwa kwa mfumo huu.

Katika mfumo huu, watendaji wa kimataifa wanaweza kuwa wahusika wa mgogoro katika kanda yetu.

Wahusika wa kimataifa mara nyingi wameonekana  kuunga mkono migogoro ya kikanda,na kuumiza kila mmoja. Wanaweza kutaka kutumia kanda fulani katika nchi ili kuwadhuru wengine katika malengo yao ya uongozi wa kifalme.

Watendaji wa kimataifa, hata kama hawana suluhisho watataka kuendeleza mgogoro na kutengeneza sera za kuendelea.

Mtazamo wa Marekani nchini Syria unalieleza hili.Watendaji mara nyingi hushabikia ugomvi kuendeela kwa nia ya wao kuendelea kuuza silaha zao.Wanaliona eneo hilo kama eneo la kibiashara na mauaji yanayozidi kuendelea hayawadhuru kwa namna yoyote.

Watendaji wa kimataifa hawawezi kudumu katika kanda moja kwa muda mrefu. Wao wanaweza kuwa si wafumbuzş wa migogoro ambayo hutokea katika nchi mbalimbali lakini hutumia migogro hiyo kwa maslahi yao binafis.Migogoro inayosababishwa na kanda katika nchi zenyewe hilo ni suala tofauti kabisa.

Ninachojaribu kukizungumzia hapa ni mbinu zinazotumiwa na watendaji wa kimataifa katika kusuluhisha migogoro hio.Mbinu hizo hazileti matokeo yanayotakikana.Mara nyingi migogoro hiyo hutangazwa lakini hufumbiwa macho.Na migogoro hiyo huzidi kuwa na utata pale tu watendaji wa kimataifa wanapoingilia kati.

Migogoro inayoendelea zaidi hufanya nchi za kikanda ziingiliwe zaidi na mataifa mengine. Pia hupunguza miaka ya kuishi watoto katika eneo na Jeografia yao na hivyo eneo hilo hushuka thamani kwa miaka mingi.Kwa hiyo, utatuzi wa migogoro ya kikanda unakuwa si rahisi na hivyo kufikia mwisho.

Dr.Kudret BÜLBÜL kutoka katika chuo kikuu cha Yildirim Beyazit amependekeza tathmini ya suala hilo.Habari Zinazohusiana