Naibu waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa Marekani yacheza na moto

Bekir Bozdağ, naibu waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa Marekani yacheza na moto kwa kushirikiana na magaidi

Naibu waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa Marekani yacheza na moto

Bekir Bozdağ, naibu waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa Marekani yacheza na moto kwa kushirikiana na magaidi

Bekir Bozdağ, naibu waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa kushirikiana na wanamgambo wa kundi la PYD/PKK sio kupambana na kundi la wanamgambo wa Daesh bali  kuunga mkono ugaidi na magaidi.

Kuundwa kwa jeshi kwa ushirikiano na wanamgambo wa kundi la PYD/YPG ambayo ni matawi ya kundi la kigaidi la PKK ili kupambana na ugaidi ni kutoa msaada kwa makundi ya kigaidi na ugaidi alizidi kusema naibu waziri mkuu wa Uturuki Bekir Bozdağ.

Bekir Bozdağ amesema kuwa kitendo cha Marekani kushirikiana na wanamgambo hao ni sawa na kucheza na moto.

Katika ukurasa wake wa Twitter Bekir Bozdağ amesema kuwa kushirikiana na kundi la kigaidi kupambana na kundi la kigaidi ni jambo lisiloeleweka.

 Habari Zinazohusiana