Balozi wa Marekani nchini Panama ajiuzulu kutokana matamshi ya Trump

Balozi wa Marekani nchini Panama John Feely  ajiuzulu kufuatia matamshi ya rais Trump kuhusu mahamiaji kutoka Afrika na Amerika-Kusini

Balozi wa Marekani  nchini Panama ajiuzulu kutokana matamshi ya Trump

 

Rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano uliofanyika ikulu Alkhamis kuhusu wahamiaji na kitambulisho cha ukaazi ambacho hutulewa kwa bahati nasibu alisema kuwa kwanini watu kutoka katika mataifa machafu wanapokelewa Marekani akimaanisha kutoka Afrika na Amerika-Kusini kuliko kuchukuwa watu kutoka nchini Norway.

Matamshi hayo yamezua ghadhabu kubwa kutoka huku na kule ulimwenguni na kumtaka rais wa Marekani Donald Trump kuamba radhi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika mitandao ya kijamii Marekani John Feely  amewasilisha barua yake ya kujşuzulu kutokana na matamshi ya Trumo kuhusu wahamiaji kutoka Afrika na Amerika-Kusini.

John Feeley aliteuliwa kuwa balozi wa Marekani nchini Panama mwaka 2015 Julia wakati wa utawala wa rais Barack Obama.

 Habari Zinazohusiana