Rais Erdoğan azungumzia mzozo wa viza kati ya Marekani na Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amesema kuwa anashangazwa kuona kuwa uamuzi wa Marekani kutotoa viza kwa raia wa Uturuki umechukuliwa na balozi wa Marekani Ankara.

Rais Erdoğan amezungumza na kusema kuwa balozi wa Ankara ana wadhifa gani mkubwa wa kuchkua uamuzi kama huo kwa niaba ya Marekani?.

Hayo rais Erdoğan ameyazungumza wakati wa mkutano wa TRT World Forum mjini Istanbul.

Kwa mujibu wa habari,rais Erdoğan amesema kuwa uamuzi kama huo kuchukuliwa na balozi unamfanya yeye kujiuliza mara mbilimbili kuhusu mahusiano kati ya Marekani na Uturuki.

Mzozo wa viza kati ya Marekani na Uturuki ulianza baada ya mfanyakazi katika ubalozi wa Marekani Ankara kukamatwa kwa madai ya kujihusisha na kundi la FETO.

Kundi la FETO ndio linashutumiwa kuhusika na jaribio la mapinduzi lililofanyika Uturuki 15 Julai 2016.Habari Zinazohusiana