Bush asema kuwa Urusi inataka kuisambaratisha Marekani

Rais wa zamani wa Marekani George W Bush amesema kuwa Urusi inataka kuisambaratisha Marekani nzima

Bush asema kuwa Urusi inataka kuisambaratisha Marekani

Rais wa zamani wa Marekani George W Bush amesema kuwa Urusi inataka kuisambaratisha Marekani nzima.

Kwa mujibu wa habari,Bush ameitaka Marekani kutoruhusu udukuzi unaofanywa na serikali ya Urusi nchini Marekani.

Ripoti zinaonyesha kuwa mtandao wa Facebook na Google nchini Marekani umedukuliwa na Urusi kwa asilima kubwa.

Marekani inaamini Urusi imetumia kampeni ya kutaka kumsaidia Donald Trump kuingia madarakani kama njia ya kufanya udukuzi nchini humo.

Bwana Bush amewataka wamarekani kuwa makini kwani jamii yao inaweza kusambaratishwa na Urusi.

 


Tagi: Urusi , Marekani

Habari Zinazohusiana