Uchambuzi wa Matukio

Uchambuzi wa Matukio

Uchambuzi wa Matukio

 

Kulingana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Ripoti ya shirika la Chakula Duniani (WFP) ya mwaka 2016, asilimia 11 ya idadi ya watu wako kwenye hatari ya njaa. Kwa hiyo watu milioni 800 wanakumbwa na janga la njaa.

Takwimu za mwaka wa 2017 zitatolewa katika miezi ijayo. Natumaini kila mtu angependelea kiwango hicho kipunguke kwa njia iliyo rahisi.

Hata hivyo kulingana na ripoti za Umoja wa Mataifa, kati ya watu watano mmoja wao anaisha katika nchi zenye migogoro  ambazo ni jambo gumu kusimamia miradi ya kilimo.

Maafa  na ukame unaokithiri kutokana na  mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakaongeza idadi hii.

Hebu tuangalie takwimu hizi , na mamia ya mabilioni ya dola yanayopotea kila kukicha:

Miezi michache iliyopita, mgogoro ulizuka baina ya Saudi Arabia na Qatar. Umoja wa falme za kiarabu , ambao ndiyo chanzo cha kueneza kila aina ya chuki kwenye nchi za kanda, wamekuwa miongoni   mwa wahusika wakuu wa mgogoro huu. Siku 10 baada ya mgogoro huo, Saudi Arabia imesaini makubaliano ya mkataba wa silaha mpya na Marekani, wenye dhamani ya dola bilioni 110.

Baada ya muda si mrefu, Qatari, mhanga  wa mgogoro huo, alitia saini na Marekani ya ununuzi wa silaha za dola bilioni 11. Nchi nyingine za ghuba zimenunua silaha zenye kiwango cha dola bilioni 200, na nchi hizo ni miongoni mwa nchi husika na mgogoro wa ghuba.

Habari kwamba utawala wa Korea Kaskazini ulijaribu makombora yake ndio habari pekee inayoshughulisha ulimwengu, na mgogoro wa Ghuba umesahaulika. Mgogoro wa korea uligonga vichwa vya habari hadi  kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-in, habari zake  zilianza kuchapishwa kila mara.

 Mtazamo wa kila habari ulikuwa ni kunadi kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini sio tishio kwa nchi yake tu, bali kwa dunia nzima.

Habari kuhusu Kim Jong kufanya majaribio mapya ya makombora kila wiki ilianza kuja. Ripoti nyingi zimeanza kurushwa na  waandishi wa habari, kama kuvamiwa na makombora kwa kisiwa cha Guam, ambacho ni maelfu ya kilomita mbali na Korea Kaskazini, kupiga mifumo ya hewa ya Kijapani na mabomu ya nyuklia juu ya nchi hii.

Baadae taarifa ziliripotiwa kwamba nchi zilizo chini ya tishio la makombora ya Korea kaskazini zilisaini mikataba ya mabilioni ya dola ya mifumo mipya ya ulinzi ili kujilinda. Jambo la ajabu na la kushangaza ni kwamba mfumo maarufu wa ulinzi wa angani wa Marekani, unaojulikana kama THAAD, ambao Wamarekani walioanzisha huko Japan, wadadisi wa mambo ya kijeshi wana wasi wasi nao kuwa hauwezi kuzuia makombora na vitisho vya  Kim Jong. Kwa upande mwingine, mazungumzo kuhusu mikataba ya mifumo mipya yanaendelea ,yako kwenye meza. Mgogoro katika eneo hili la Asia ya Pasifiki pia imesababisha mamia ya mabilioni ya dola kuhamishiwa na kutumiwa kwenye biashara za silaha.

Moja ya vikosi 9 vya Marekani vilioko nje yake, ni kikosi kilioko Asia ya Pasifiki (PACOM). Kikosi hicho kiko Hawaii, na kina sehemu kubwa ya bajeti ya PENTAGON. Na sifa za kikosi hiki, ni kuwa kin aza kisasa na mafunzo ya hali ya juu.

Kikosi cha Marekani kwenye eneo la Asia ya Pasifiki kimejidhatiti na teknolojia ya kisasa, ndege za kizazi cha 5 aina ya F-35, ndege zisizokuwa na marubani aina ya  "Eagle Grey", bila kusahau manuari zenye uwezo wa nyuklia. Vifaa vyote hivyo vilitumwa Korea ya Kusini na Japani. Marekani ilituma pia  askari 75,000 kwenye eneo hilo.  

Jambo gani linaendelea ? Kuanzia Iran hadi India, mpaka kwenye visiwa vidogo vya pasifiki, nchi nyingi zimefungulia milango na kupokea kwa mikono miwili makampuni ya silaha ya Marekani na Urusi. Tena miakataba ya silaha yenye dhamani ya mamia ya mabilioni imesainiwa.

Mwaka uliopita, pesa iliotumiwa kwenye maisha ya kifahari  ni karibu dola bilioni 1.1. Kila mwaka, ulimwenguni huzalishwa chakula kinachotosha kuwalisha walimwengu, ila kwa bahati mbaya, idadi kubwa ya chakula hiki huharibiwa kutokana na israf. Tani bilioni 1.3 za chakula pia hupotea kutokana na ukosefu wa mipango  ya fedha, ya kiufundi na tahadhari za chakula. Nchini Marekani pekee, kiasi cha chakula kilichoharibika ni tani milioni 222. Kiasi hiki kinatosha kulisha Afrika yote.

Kwa upande mwingine, hatupaswi kusahau mamia ya mabilioni ya dola tunayolipa kwa vipodozi vinavyoharibu hali ya hewa.

Wataalamu wa kilimo wanasema kuwa mgogoro wa Korea na Ghuba, na fedha zilizowekwa mikononi mwa nchi, zinatosha kuwalisha watu waliokufa kwa njaa kwa kipindi cha miaka 10.

 Habari Zinazohusiana