İstanbul kuwa mwenyeji wa kongamano la masuala ya kimataifa Oktoba 18

Istanbul yaanda kongomano kuhusu masuala ya kimataifa ifikapo Oktoba 18 mwaka 2017

İstanbul kuwa mwenyeji wa kongamano la masuala ya kimataifa Oktoba 18

 

Shirika la habari la Uturuki TRT world linalo peperusha habari kwa lugha ya kiingereza litapeperusha kongamano ambalo litazungumzia masuala ya kimataifa ifikapo Oktoba 18.

Kongamano hilo kuhusu masuala tofauti  ikiwa utamaduni, siasa, uchumi na jamii yatajadiliwa  katika kongamano hilo.

Watu zaidi ya 400 miongoni mwao  wanasiasa, wasomi, wanaharakati na waandishi wa habari watashiriki katika kongamano hilo.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni mabadiliko katika wakati mgumu.

Kongamano hilo la TRT World limewaarifu watu mashuhuri kama kiongozi Jose Luis Rodriguez Zapatero, mtoto wa kike wa Malcolm X kwa jina Ilyasah Shabazz,  waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu, kiongozi kutoka Afrika Kusini Bathabile Olive Dlamini, mkurugenzi  wa kituo cha habari cha TRT World  İbrahim Eren  na  Karin von Hippel .

Mkutano huo utazungumzia masuala ya kisiasa na wajibu wa vyombo vya habari kutatua mizozo mbali mbali.

Majadiliano yataangazia hasa masuala kama vile ubaguzi  wa rangi, chuki dhidi ya Uislamu, uvunjwaji wa haki za binadamu na migogoro ya kimataifa.

Vile vile njia za ufumbuzi wa matatizo tofauti zitapendekezwa.

Pamoja na uzinduzi wa mradi wa "TRT World Citizen" utakaofanyika jioni ya tarehe 18 Oktoba, mradi wa TRT World Citizen utaanzisha mipango ya kupatia jawabu ya mizozo ya kijamii.

Mojawapo ya miradi hiyo ni kusaidia watoto waliotenganishwa na wazazi wao kutoka na vita kwenye maoneo tofauti ulimwenguni.

 Pia kutakuwa makala maalum itakomulika madhila yanaowakumba wakimbizi.

Mkurugenzi wa kituo cha habari cha TRT, Fatih Er alisema kuwa watandaa makala maalum kuhusu watoto wahanga wa biashara haramu ya viungo vya binadamu pamoja na vipindi kuhusu mizozo ya kijamii na ufumbuzi wake. 

Mengi zaidi kuhusu kongomano hilo yanapatikana forum.trtworld.com

 

 Habari Zinazohusiana