Watoto 19 huuawa au kujeruhiwa kila siku kwa risasi nchini Marekani

Utafiti wadhihirisha kwamba kila siku watoto 19 huuawa au kujeruhiwa kwa risasi nchini Marekani

Watoto 19 huuawa au kujeruhiwa kila siku kwa risasi nchini Marekani

Utafiti wadhihirisha kwamba watoto nchini Marekani hasa watoto weusi wamo hatarini baada ya kudhihirika kwamba kila siku watoto 19 huuawa au kujeruhiwa kwa risasi nchini humo.

Takwimu zimeonyesha kwamba ripoti iliyotolewa ya kati ya mwaka 2002 hadi 2014 imeonyesha kwamba uhalifu wa mitaani kwa kutumia bunduki umedhihirisha kuwa na 'Mzozo wa kiafya' nchini humo.

Ripoti hiyo ilitolewa baada ya utafiti kufanywa kwa kukusanya vyeti vya waliofariki pamoja na majeruhi waliopelekwa hospitali kwa dharura .

Ripoti hiyo pia imeonyesha kwamba mauaji mengi ya kutekelezwa kwa risasi yamefanywa kwa kusudi huku zingine zisizokuwa kwa kusudi.

Mauaji yaliyosababishwa kwa kupiga risasi bila ya kukusudia yameonekana kusababishwa na mchezo wa kutumia bunduki iliyo na risasi.

 Habari Zinazohusiana