Urusi yatoa wito kwa Marekani kuheshimu mamlaka ya Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi aitaka Marekani kuepuka hatua za kulenga upande mmoja pekee nchini Syria

Urusi yatoa wito kwa Marekani kuheshimu mamlaka ya Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov atoa wito kwa nchi zote hasa Marekani kuheshimu mamlaka na hadhi ya nchi ya Syria .

"Ni muhimu kabisa kuheshimu hadhi,mamlaka na mipaka ya nchi ya Syria kama vile ilivyoelezewa na Baraza la Usalama la UN katika azimio la 2254."

Lavrov amesema haya baada ya jeti ya jsehi la majini la Marekani kushambuliakwa risasi  jeti ya vikosi vya utawala mapema siku ya Jumatatu.

Lavrov alikuwa anaongeana waandishi wa habari  katika mkutano na mawaziri wengine wa nchi ya Brazil, India, China na Afrika Kusini jijini Beijing .

Aidha mwanadiplomasia huyo wa Urusi alisema kwamba kuwepo kwa maeneo salama Syria ni njia mbadala muhimu ya kucchukuliwa .

 Habari Zinazohusiana