Marekani yahofia shughuli za ushirikiano baina ya Uturuki na Urusi

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani afahamisha kwamba anahofia ushirikiano unaoendelea baina ya Uturuki na Urusi

Marekani yahofia shughuli za ushirikiano baina ya Uturuki na Urusi

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson wiki iliyopita alielezea wasiwasi wake wa Uturuki kuhusisha Urusi katika masuala tofauti bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu hofu aliyo nayo.

Mwishoni mwa wiki hii Daily Sabah ,gazeti la Uturuki lilijaribu kutafuta majibu kuhusu kauli ya Tillerson baada ya kujaribu kumhoji mmoja ya wasemaji wa wizara hiyo ya Marekani bila ya mafanikio.

Msemaji huyo alidai kwamba wizara ya mambo ya nje haina fursa ya kutoa majibu kufuatia kauli ya waziri wake .

Hii ni mara ya kwanza kauli kutoka serikali ya Donald Trump kuhusu uhusiano baina ya Uturuki na Urusi imefanyika .

 

 Habari Zinazohusiana