Mtazamo wa Uturuki Mashariki ya Kati

Mtazamo wa Uturuki Mashariki ya Kati

Mtazamo wa Uturuki Mashariki ya Kati

 

Saudi Arabia,Milki za Kiarabu na Misri ikiwa ni pamoja na mataifa mengine ya ghuba ya kiarabu yaliungana na kuwekea vikwazo Qatar ikiwa5,2

3, ni pamoja na kukata uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi hiyo katika kanda hiyo.

Wiki hii katika kipindi cha mtazzmo wa Uturuki Mashariki ya Kati tutaangazia mzozo wa Qatar.

Kutoka cchuo kikuu cha Atatürk kitengo cha uhusiano wa kimataifa Cemil Doğaç İpek anatoa tathmini ya kipindi hetu cha leo.

Kwa muda wa wiki moja sasa kanda ya ghuba ya kiarabu inakumbwa na mzozo mkubwa baada ya Saudi Arabia,Bahrain,Milki za kiarabu na Misri kuanzisha shutuma dhidi ya Qatar kwa kuunga mkono ugaidi na kutoa msaada kwa baadhi ya makundi ya kigaidi jambo ambalo lilipelekea  nchi hizo kuchukua hatua ya kukata uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo.Hatua ya kusitisha kabisa uhusiano wa kidiplomasia na Qatar ulipelekea Marekani kushinikiza mataifa ya ghuba kuhusu kusahihisha uhusiano wake na Qatar.Licha ya kuwa shutuma hizo za ushirikiano na ugaidi bado nchi hizo hazijatoa ushahidi  wa kuthibitisha madai yao.

 

Qatar ni nchi ndogo katika ghuba ya uajemi ingawaje ina ushawishi mkuu katika siasa na uchumi katika kanda hiyo.Kuna jumla ya watu milioni 3 wanaoishi Qatar,na elfu 330 ni raia asilia wa Qatar.Pia nchi hiyo ni ya tatu kwa kuwa na hifadhi kubwa zaidi ya gesi asilia dunian.Isitoshe Qatar ni mwenyeji wa baadhi ya taasisi muhimu sana za elimu,makampuni na pia shirika la habari la kimataifa la Al Jazeera .Jeshi kadhaa za mataifa ya kigeni pia zinapatikana katika ardhi ya nchi hiyo.Baada ya Qatar na Uturuki kutia saini mkatab awa ushirikiano wa kiuchumi,sekta ya kijeshi na pia mikataba mingine mataifa kadhaa ya ghuba ya kiarabu yameonekana kutoridhishwa na hatua hizo.

Qatar ni nchi tajiri zaidi katika ghuba na pia nchi muhimu san akwakuwa imekuwa ikiuunga mkono harakati za kidemokrasia katika kanda hiyo.Ni nhci ambayo ina ushawishi mkubwa si katika nyanja za kiakanda peke bali pi aza kimataifa hasa kwa kuwa na shirika la vyombo vya habari la Al Jazeera .Al Jazeera hupeperusha habari zake kwa lugha ya Kiarabu na Kiingereza .

Qatar husisitiza zaidi usimamizi huru katika serikali kuliko serikali zingine zote za mataifa ya ghuba.Sababu kuu ya hatua ya mataifa ya ghuba dhidi ya Qatar ni kwa kuwa nchi hiyo imekuwa ikiuunga mkono baadhi ya wanaharakati wa upinzani wa baadhi za nchi hizo.Aidha pia kwa kuwa sera za serikali ya Doha zitakuwa na madhara katika sera zingine za kimataifa.Tuna ufahamu kwamba Uturujki na Qatar zinaunga mkono upinzani Syria dhidi ya utawala wa Assad.Qatar na Uturuki pia walisisitizia upinzani wa Syria kuka katika meza za mazungumzo ya amani Geneva na Astana .       

Vikwazo vilivyoekewa Qatar,ambayo ni mwanachama wa muungano wa mataifa ya OPEC yanayofanya uuzaji wa nje wa mafuta umepelekea kuwa na bei za juu za mafuta .Sasa bei ya mafuta aina ya Brent Petroli imependa kwa asilimia 2 na kupelekea bei yake kuwa zaidi ya dola 50.Hii ina maana kwamba mzozo katika kanda hiyo ukiendelea Qatar yaweza chukua hatua ya kujitoa OPEC.Kanda ya ghuba haipo tayari kuwa na mgogoro mwengine tena .Hata hivyo kuna uwezekano kuwe na mgogoro katika kanda hiyo kwa mtazamo wa serikali ya Saudi Arabi ana sera inazoendeleza Yemen .Hii inaweza kupelekea hata vita vya kikanda .

Kulingana na sera za kigeni za Uturuki kwa sasa itabidi itupilie mbali mitazamo ya tofauti za kidhehebu kama za Shia na Sunni.Kwa sasa itaonyesha urafiki wake na nchi ya Qatar,kwa kuwa ni mojawapo ya marafiki muhimu katika ghuba hiyo.Rais Wa Uturuki amekuwa mstari wa mbele kuendeleza juhudi za kidiplomasia kusuluhisha mzozo wa Qatar.Hatua kadhaa za kidiplomasia zilizochukuliwa na rais Recep Tayyıp Erdoğan kufuatia mzozo huo zimeonyesha kuwa na matumaini.Hatua hizo zizlizohukuliwa tangu kuanza kwa mzozo huo zimezuia mgogoro huo kutoendelea kuwa mbaya .

Uturuki ina mtazamo wa kwamba ustawi wa kanda hiyo ni kuwa na ustawi Uturuki pia.Uturuki inapendekeza kuwe na ushirikiano katika kanda hiyo ili kuweza kupiga vita ugaidi na makundi kama Daesh,chuki dhidi ya uislamu,m,gawanyiko ya kidhehebu na migawanyko ya kijamii.Uturuki imeahidi kutoa msaada wa aina yoyote ili kuhakikisha hali ya kawaida inarudi katika kanda hito ya ghuba .

 

                                                                

 Habari Zinazohusiana