Qatar yatoa shukrani kwa Uturuki

Chumba cha biashara cha Qatar chatoa shukrani kwa Uturuki kwa kutuma bidhaa zake baada ya vikwazo

Qatar yatoa shukrani kwa Uturuki

 

Chumba cha biashara cha Qatar chatoa shukrani kwa Uturuki kwa kutuma bidhaa zake baada ya vikwazo

Mkurugenzi mkuu wa chumba cha biashara cha Qatar  Salih Hamad el Sharki ametoa shukrani kwa Uturuki kwa kuweza kupeleka bidhaa zake nchini Qatar.

Qatar ilikumbwa na uhaba wa bidhaa tofauti baada ya kuwekewa vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi na baadhi ya mataifa ya Ghuba Juma lililopita.

Uturuki alichukuwa uamuzi wa kutuma bidhaa ya chakula ili kukidhi mahitaji ya kwanza ya raia wa Qatar.

Mkurugezni huyo alizungumzia kuhusu athari za vikwazo vilivyochukuliwa na mataifa ya Ghuba yakishinikizwa na Saudia Arabia.

Mkurugenzi huyo ametoa shukrani kwa Uturuki  kwa bidhaa hizo  na kuimba kuzidi kuwa kimoja na ushirikiano.


Tagi: Qatar , Uturuki

Habari Zinazohusiana