Juhudi kutoka Uturuki ili kuzuia mzozo wa Qatar

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım asema kuwa rais Erdoğan anatumia juhudi ili kuzuia mzozo wa Qatar kuendela

Juhudi kutoka Uturuki ili kuzuia mzozo wa Qatar

 

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım asema kuwa rais Erdoğan anatumia juhudi ili kuzuia mzozo wa Qatar kuendela

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım asema kuwa rais wa Uturuki  Recep Tayyıp Erdoğan anatumia juhudi kubwa ili kuzuia mzozo wa Qatar kuendelea.

Waziri mkuu wa Uturuki amezungumza kuhusu mzozo wa Qatar na baadhi ya mataifa ya Ghuba baada ya kutangaza ushirikiano wa kidiplomasia na Doha.

Waziri mkuu wa Uturuki alitoa salam za rambi rambi kwa Azerbaijan kufuati kifo cha waziri wa nishati Natig Aliyev.

Hafla ya iftar iliandaliwa katika ofisi ya waziri mkuu mjini Istanbul.

Katika hotuba yake waziri mkuu wa Uturuki alisema kuwa kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliotokea Baghad, Kabul, Ufilipino, London na Tehran katika siku za nyuma ni wazi kuwa hakuna taifa lililosalama na matendo ya kigaidi.

Waziri mkuu ameyataka mataifa yote kuwa kitu kimoja na kuwa na msimamo mmoja dhidi ya matendo ya kigaidi.

Akizungumzia kuhusu ghasia na machafuko Mashariki ya Kati na mzozo wa Syria, Iraq, Yemen ikiwemo Libya amesema kuwa kuhusu mzozo wa Qatar na mataifa ya Ghuba utapatiwa suluhu kwa njia ya mazungumzo.Habari Zinazohusiana